RAIS
Jakaya Kikwete (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia
katika sherehe za wafanyakazi, Mei Mosi zitakazofanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Hezron Kaaya
mapema wiki hii aliwaambia wanahabari kuwa maadhimisho ya Sikukuu ya Mei
Mosi mwaka huu yatafanyika kitaifa katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es
Salaam.
“Katika
kikao chetu na Rais Kikwete alishangaa kuona kuna mambo bado yamelala
licha ya kuwa yameshafanyiwa kazi. Kuna suala la ukokotoaji kwa mifuko
yote ya jamii kutofanyiwa kazi licha ya kuwa tayari wamefanya tathmini,
lakini bado linasuasua,” alisema.
Alisema
Rais pia alishangaa kwamba suala la kodi linaendelea kuwalemea
wafanyakazi wachache walioko katika sekta rasmi na kuacha wengine wakiwa
hawalipi kodi kwani nguvukazi ya nchi ni zaidi ya watu milioni 21,
lakini wanaotozwa kodi ni milioni tatu pekee.
Aliongeza
kuwa leo kutakuwa na maandamano ya wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali
nchini ambayo yataanzia Mnazi Mmoja na kuishia katika uwanja huo wa
Uhuru yatapokelewa na Rais Kikwete ambaye atazungumza na wafanyakazi hao
Post a Comment