Mganga
Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo (kulia) akizungumza na
mwandishi wa habari hizi. Kushoto ni mmoja wa manesi wa kituo.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Sehemu ya jengo la Kituo cha Afya Simambwe, likitoa huduma.
BAADHI
ya akinamama na wanakijiji wa baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela
Wilaya ya Mbeya Vijijini wamewalalamikia wauguzi na wahudumu wa afya
katika Kituo cha Afya Simambwe kwa kile baadhi yao kuwaomba kitu kidogo
(rushwa) hasa kwa wajawazito wanapofika katika kituo hicho kupata
huduma.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake kutoka vijiji vinavyohudumiwa na
kituo hicho vya Usoha Njiapanda, Shibolya, Simambwe, Garijembe, Ilembo
Usafwa, Ngoha na Zunya walisema mjamzito amekuwa akiombwa kutoa shilingi
2000 kila anapojifungulia nyumbani kwa dharura baada ya kushindwa
kufika katika kituo hicho.
Mmoja
wa akinamama aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye aliomba
kutotajwa kwa kuwa huenda akapata taabu kihuduma za afya kituoni hapo,
alisema kwa sasa ni jambo la kawaida wahudumu kuwaomba chochote
wajawazito kituoni hapo.
“…Unajua
vijiji vingi vinavyohudumiwa na kituo hiki vipo mbali na miundombinu ya
barabara si mizuri, yaani hakuna usafiri zaidi ya bodaboda ambazo
lazima zitoke Simambwe…sasa kutokana na hali hii inatokea mjamzito
anajifungulia nyumbani kwa msaada wa wakunga wa jadi, akipeleka mtoto
huyo kituo cha afya basi wanamuomba shilingi 2000 haijulikani ya nini,
sasa hili si tunaamini sio haki,” alisema mama huyo.
Aidha
baadhi ya wanakijiji walikilalamikia kituo hicho kwa kitendo cha
kulalamika muda wote hakina dawa huku wahudumu wakiwaelekezwa kwenda
kununua dawa jambo ambalo wanahisi kuna mchezo mbaya unafanywa na
wahudumu hao.
“Muda
wote ukienda kutibiwa utasikia kauli za hakuna dawa tunakuandikia nenda
kanunue, tena wengine wanaelekeza hadi maduka ya kununua dawa hizo ndio
maana baadhi yetu tunahisi kuna mchezo mbaya (kuhujumu dawa) unaofanywa
na baadhi ya wahudumu.,” alisema Mzee aliyejitambulisha kwa jina la
Kalamwa.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo
alipinga vikali uwepo wa vitendo vya kuomba rushwa kwa watumishi wa
kituo hicho na kudai malalamiko kwa wanachi wanaohudumiwa na kituo hicho
imekuwa kitu cha kawaida hasa wanapotembelewa na mgeni.
“..Hakuna
kitu kama hicho unajua wakazi wengi wa vijiji hivi wamezoea kulalamika
hasa wanapotembelewa na mgeni…hakuna wanaoombwa fedha, mjamzito
akijifungua nyumbani tunampokea bila masharti na kumpatia huduma
anazostahili, si kweli wanachokilalamikia,” alisema Mwaipopo.
Hata
hivyo alisema kituo hicho kinahudumia idadi kubwa ya watu zaidi ya
uwezo wake jambo ambalo hukifanya kuelemewa kwa idadi ya dawa
wanazoletewa, wahudumu na vifaa vingine tiba hivyo kuiomba Serikali
kukiongezea mgao wa dawa.
“…Kituo
kinahudumia idadi kubwa ya watu kupita uwezo wake hivyo unakuta hata
baadhi ya changamoto kama ufinyu wa dawa na wahudumu vinatokana na hali
kama hiyo…,” alisema Mganga huyo Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TGNP
Post a Comment