Wachezaji wa Manchester United wakisikitika baada ya kipigo leo
GUNDU
bado lipo Manchester United licha ya kubadilisha kocha, baada ya jioni
hii kufungwa bao 1-0 na Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu ya England
uliofanyika Uwanja wa Old Trafford.
Kipigo
hicho katika mchezo wa pili wa Ryan Giggs tangu arithi mikoba ya David
Moyes, kinaipa ahueni Sunderland na kuipeusha kwenye balaa la kushuka
daraja.
Lilikuwa
ni bao pekee la Sebastian Larsson dakika ya 30 ambalo leo hii
limeirejesha Man United katika zama za vipigo chini ya Moyes, huo ukiwa
ushindi wa kwanza wa Sunderland Uwanja wa Old Trafford tangu mwaka 1968.
Sebastian Larsson akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la ushindi Sunderland
Makocha wapya, gundu pale pale: Kocha Mkuu, Ryan Giggs na wasaidizi wake Nicky Butt na Paul Scholes leo
Post a Comment