Na Father Kidevu Blog
SHINDANO
la Miss Dar City Center limezinduliwa rasmi jana na linatarajiwa
kufanyika mei 24 kwaka huu katika ukumbi ambao utatangazwa baade, huku
likishirikisha warembo 15.
Akizungumza
katika uzinduzi huo jana, mratibu wa shindano hilo, Judith Charles
alisema kuwa, mwaka huu shindano hilo litambapwa na vionjo tofauti
tofauti ili kulifanya kuwa la aina yake.
Judith
alisema kwamba, wameangalia changamoto zilizotokea kwa waandaaji wa
waliopita wa shindano hilo, ili kuweza kulifanya kuwa na ubora wa hali
ya juu zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.
“Tumetumia changamoto ya waandaaji waliopita wa shindano hili
na sisi tumeamua kuliboresha zaidi na hivyo tunaamini kabisa kwamba litakuwa
katika kiwango cha juu zaidi tofauti na uilivyokuwa hapo mwanzo,” alisema
Judith.
na sisi tumeamua kuliboresha zaidi na hivyo tunaamini kabisa kwamba litakuwa
katika kiwango cha juu zaidi tofauti na uilivyokuwa hapo mwanzo,” alisema
Judith.
Aidha
aliongeza kusema kwamba, ana aimani kubwa kwamba Miss Dar City Center
ndiko atakakotokea Miss Tanzania 2014, kwani wamejiandaa kwa ukamilifu
wa hali ya juu.
Judith
alisema kwamba ana imani kubwa na matron ambaye pia ndie mwalimu wa
warembo wa shindano hilo, Eshe Rashid kuwa atawapa mafunzo mazuri zaidi
yatakayowezesha kuwa bora zaidi jukwaani.
Pia
aliongeza kusema kwamba, zawadi kwa washindi wa shindano hilo zitakuwa
zimeboreshwa zaidi na hivyo ana imani zitavutiwa zaidi na warembo hao.
Aidha
Judith alisema, shindano hilo kwa kiasi kikubwa linafadhiliwa na
Prima, Zanzi, Sky light band, Clouds FM, Dimond Bureu De Change LTD,
gazeti la Jambo leo, Klabu Maisha ambako warembo wanafanyia mazoezi,
blog ya Wananchi, blog ya Father Kidevu,
Hoteli ya JB Belmont na Machapta Production
Hoteli ya JB Belmont na Machapta Production
Post a Comment