Mwili wa marehemu PC JUMANNE ukishushwa kupelekwa ukumbini kwa ajili
ya kuagwa
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora ACP. Suzan Kaganda jana tarehe 30/04/2014
jioni amewaongoza waombelezaji na watendaji kutoka vyombo vya usalama,
askari, taasisi za serikali na zisizo kiserikali za mkoa wa Tabora
kuuaga mwili wa Askari PC JUMANNE ambaye aliyefariki baada kupigwa
risasi na majambazi akiwa katika majukumu ya utendaji kazi.
RPC Tabora ACP. Suzan Kaganda akiongoza waombelezaji kuaga mwili wa
marehemu PC JUMANNE.
Waombelezaji wakiwa katika hali ya majonzi
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tabora wakiwa katika hali ya huzuni.
Mchungaji wa Kanisa la Waadivensti akiongoza misa
Post a Comment