Toka
March 8 2014 mpaka leo ikiwa ni May, ndege ya Malaysia iliyokua imebeba
zaidi ya watu 200 haijulikani ilipo baada ya kupotea ikiwa inatokea
Malaysia kwenda Beijing China.
Kwa
siku zote hizo toka imepotea ndugu waabiria wa ndege hiyo wamekua
wakishinda kwenye hoteli ambazo pia zimekua zikitumiwa na shirika hilo
la Malaysia kukusanyika na kutoa taarifa kuhusu kinachoendelea kwenye
kuitafuta ndege hiyo.
May 1
2014 taarifa zimeanza kusambaa kwamba ndugu hao sasa wamepewa maagizo
waondoke kutoka kwenye hoteli zote walizofikia Beijing na Kuala Lumpar
na kurudi nyumbani kwao ambapo taarifa za chochote kitakachotokea
watazipata wakiwa hukohuko majumbani.
Hii
iliwafanya ndugu kadhaa kuangua tena vilio na kupiga mayowe baada ya
kujua kwamba taarifa ya shirika hilo la ndege inamaanisha haitakuwepo
tena ile mikusanyiko ya kila siku kwenye chumba cha mikutano kwa ndugu
hao kupewa taarifa za kinachoendelea kwenye zoezi la utafutaji wa ndege
hiyo.
Kwenye
hoteli ya Lido Beijing ambako kampuni hiyo ya ndege imekua ikiwalipia
ndugu hao wa abiria toka ndege ipotee, kulikua na watu wanaozidi 500
ambao wote ni ndugu wa abiria waliopotea.
Hata
hivyo kampuni hii ya ndege itaanza kutoa malipo ya pesa kwa ndugu hao
siku za karibuni ambapo japo haijasema itatoa kiasi gani, sheria inasema
ndugu wanaweza kulipwa kuanzia dola za kimarekani laki moja na nusu
mpaka laki moja na elfu 75.
Ripoti
mpya iliyotoka inasema maafisa hawakua wamegundua kupotea kwa ndege
hiyo mpaka dakika 17 baadae na walichelewa kwa dakika 240 kuanza
kuitafuta ndege hiyo baada ya kupotea kwenye radar.
Post a Comment