Askofu
Gervas Nyaisonga wa jimbo la Katoliki la Mpanda akisalimiana na Mapadri
wa jimbo hilo katika eneo la mto koga Hapo jana ambapo ndipo
linapoanzia Jimbo katoliki la Mpanda wakati alipokuwa akiwasili rasmi
kwenye jimbo lake jipya la Mpanda akiwa anatokea jimbo la Dodoma
Askari wa
skauti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda wakiwa katika eneo la daraja
la mto koga wakimpokea askofu Gervas Nyaisonga alipowasili hapo jana
akitokea jimbo la Dodoma ambapo askofu Nyaisonga alipokuwa analiongoza
kabla ya kuhamishiwa Jimbo la Mpanda na amesimikwa jana kuwa askofu wa
Jimbo la Mpanda
Askofu
Gervas Nyaisonga wa Jimbo katoliki la Mpanda akibusu Ardhi hapo jana
katika kijiji cha Kamsisi ikiwa ni ishara ya kuhamia rasmi kuliongoza
jimbo la Mpanda akitokea jimbo katoliki la Dodoma
Msafara
wa waendesha pikipiki wakiwa katika eneo la uwanja wa ndege mjini
Mpanda wakiwa wanaongoza msafara wa kumpokea askofu Gervas Nyaisonga
hapo jana ambae amehamishiwa jimbo la Mpanda akitokea jimbo la dodoma
Mapadri
wa kanisa katoliki wakiwa kwenye kanisa kuu la jimbo Katoliki la Mpanda
kabla ya kuanza kwa ibada ya kukabidhiwa ufunguo wa kanisa hilo askofu
Gervas Nyaisonga ambae amehamishiwa jimbo la Mpanda ikiwa ni ishara ya
kuyaongoza makanisa na kuyasimamia makanisa yote ya jimbo katoliki la
Mpanda
Picha na Walter Nguluchuma
Katavi yetu Blog
******************
Na Walter Mguluchuma
Padri wa
Kanisa Katoliki wa Jimbo la Mpanda Padri Matini Kapufi (42 ) pamoja na
Katekista wa Kanisa hilo wa KijiJI cha mtakuja Parokia ya
Inyonga Katekista Patricki Mwendo wa Saa (60)
wamefariki Dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kupinduka baada ya gari kuacha njia na watu wengine wawili kujeruhiw
na kulazwa hospitalini
Kwa
mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi
Dhahiri Kidavashari ajari hiyo ilitokea hapo juzi majira ya saa nne
asubuhi katika Kijiji cha Kamsisi tarafa ya Inyonga
barabara ya Inyonga kuelekea Mkoani Tabora
Alisema
ajari hiyo ililihusisha gari aina ya Toyota Hilux pick
Up lenye namba za usajiri T 302 CUY lililokuwa likiendeshwa
na Marehemu Padri Martini Kapufi ambae ni Paroko wa parokia ya
Mwese jimbo katoliki la Mpanda
Kidavashari aliwataja
watu waliojeruhiwa kwenye ajari hiyo kuwa ni Daud
Saveli (31) katekista msaidizi wa kijiji cha Mtakuja parokia ya
Inyonga, ambae ameumia sehemu ya kidevu chake na mguu wa kushoto na
melikio Maraluma mkazi wa kiji cha mtakuja Tarafa ya Inyonga Wilaya ya
Mlele
Alisema watu
hao walipata ajari wakati wakiwa wanasafiri kutoka Inyonga makao
makuu ya Wilaya ya mlele wakiwa wanaelekea eneo la Mto Koga
mpakani mwa Mkoa wa Katavi na Tabora kwa lengo la kwenda kumpokea
Askofo Gervas Nyaisonga aliyekuwa akitokea Dodoma ambae ameamishiwa
jimbo la Mpanda akitokea jimbo katoliki la Dodoma
Kamanda
Kidavashari alieleza kuwa watu hao ndipo walipokuwa wakisafiri na
gari hiyo na walipofika katika maeneo ya kijiji cha Kamsisi gari hiyo
iliacha njia na kupinduka ambapo Katikista Patrick Mwendowasaa
alifariki hapo hapo mara baada ya kutokea kwa ajari na Padri Martini
Kapufi alifariki njiani wakati akiwa anapelekwa kwenye kituo cha
afya cha Inyonga
Alisema
majeruhi wote wawili wamelazwa katika kituo cha afya cha
Inyonga wakiwa wanaendelea kupatiwa matibu huku hali zao zikiwa
zinaendelea vizuri na miili ya marehamu hao wawili imehifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo cha afya cha Inyonga
Kamanda
Kidavashari alieleza kitengo cha jeshi la polisi kikosi cha usalama
barabarani kinaendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo
kilichosababisha ajari hiyo ya gari mali ya jimbo Katoloki la Mpanda
Post a Comment