“PRESS RELEASE”TAREHE 04.05.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHAN
GARI
YENYE NAMBA ZA USAJILI T.939 ANC AINA YA TOYOTA MARK II ILIYOKUWA
IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA ILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI
ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.101 CRS AINA YA
DAYUNI AITWAYE ERASTO DAUDI (23) MKAZI WA PAMBOGO NA KUSABABISHA KIFO
KWA ABIRIA WA PIKIPIKI HIYO AITWAYE NATHANIEL VITUS (23) MKAZI WA
PAMBOGO NA MAJERAHA KWA DEREVA WA PIKIPIKI HIYO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO ENEO LA
SOWETO, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MAJERUHI
AMELAZWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA
ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA KULITELEKEZA GARI ENEO HILO. JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MSAKO:
WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.YOHANA FAUSTINE (21) NA 2. SHABANI
MSEWA (20) WOTE WAKAZI WA UHAMILA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI KETE 09 SAWA NA UZITO WA GRAMU 45.
WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:40 JIONI HUKO
KATIKA KITUO CHA POLISI RUJEWA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI
MKOA WA MBEYA. AWALI WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KWA KOSA LA KUINGIA
HIFADHI YA TAIFA IKONGA BILA KIBALI NA WAKATI WANAPEKULIWA KABLA YA
KUINGIA MAHABUSU WALIKUTWA WAKIWA NA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment