WATU
saba wakiwemo wafanyakazi wawili wanawake wa benki ya Barclays
wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kula
njama na unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na wiza wa sh milioni
390.2 , dola za kimarekani 55,000 na Euro 2150.
Washtakiwa
hao ni Alune Kasililika (38), Neema Batchu (26) wafanyakazi wa benk
hiyo, Kakame Julius (38), Iddy Khamis (32), Sezary Msolopa (31),
Boniphace Muumba (29) na Ruth Macha (30) wafanyabiashara.
Wakisomewa
mashitaka yao mbele ya hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba ambapo Wakili
wa Serikali Tumaini kweka akisaidiana Mwanaamina Kombakono walidai
kuwa wastuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili.
Aliieleza
mahakama kuwa katika tarehe tofauti zisizo fahamika washtakiwa wakiwa
ndani ya jiji la Dar es Salaam walikula njama kwa nia ya kutenda kosa
la wizi.
Katika
shtaka la pili washtakiwa wanadaiwa kuwa Aprili 15 mwaka huu, wakiwa
katika benki hiyo tawi la Kinondoni, Dar es Salaam waliiba fedha
tasilimu sh.
milioni 390.2, Dola za Marekani 55, 000 na Euro 2150 mali ya Barclays.
Hata
hivyo, ilidaiwa kuwa kabla ya kufanya wizi huo walimtishia kwa silaha
Anifah Ahmad na Anna Tegete ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo ili
kuweza
kujipatia na kumiliki fedha hizo.
Baada
ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo walikana kuhiska na tukio hilo,
ambapo wakili Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika
wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu
Mwaseba alisema kwa mujibu wa sheria shtaka la pili halina dhamana, kwa
hiyo washtakiwa watakuwa chini ya ulinzi na kupelekwa gerezani hadi Mei
15 kesi hiyo itakapotajwa.
mwaka huu.
Katika
tukio hilo ilielezwa kuwa majambazi hao walifika katika benki hiyo
Aprili 15, mwaka huu, saa 9:00 mchana wakiwa na magari mawili na bunduki
aina ya SMG pamoja na bastola, kisha waliingia ndani ya benki hiyo na
kupora fedha walizotoka nazo kwenye mfuko na kukimbia nazo kwa kutumia
pikipiki.
Hivi
karibuni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemain Kova
akizungumza tukio hilo alisema kuwa wamegundua baadhi ya matukio ya wizi
wa fedha unafanywa na wafanyakazi wa benki.
Alisema
katika wizi huo, robo tatu ya fedha zote zilizoibwa zilichukuliwa siku
moja kabla ya tukio linalodaiwa kutengenezwa la wizi, kwa lengo la
kuficha wizi huo na kwamba kulikuwa na vikao mbalimbali vya maandalizi
ya kufanikisha tukio hilo.
Alisema Aprili 15, mwaka huu siku ambayo wizi huo unatajwa kufanyika, kilichotokea ni tukio la kukamilisha njama hizo.
“Tukio
hili lilileta utata tangu mwanzo tulipokwenda kukagua eneo la tukio,
kwani siku moja kabla, yaani Aprili 14, gari la kubebea fedha kupeleka
Benki Kuu lilifika katika tawi hilo kama ilivyo kawaida lakini fedha
hazikutolewa kumbe ilikuwa ni mkakati uliowekwa kufanikisha wizi huo.”
Post a Comment