Juhudi
za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan
ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko
ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji
hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa wa karibu mita kumi kwenda juu
baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja kutokana na mvua kubwa
zinazonyesha.
Miili
ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana katika maporomoko ya ardhi
kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana
akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana makazi.
Mashirika
ya misaada na uokoaji kwa sasa wameanza kuwapa mikate na maji maelfu ya
watu waliolala nje kwenye baridi kali wakiwa hawana makazi.
Kuna
taarifa nyingine zinazosema maelfu mengine ya watu huenda wakawa
wametoweka baada ya upande mmoja wa mlima kuangukia kijiji k katika eneo
la mashambani la mkoa wa Badakhshan unaopakana na mataifa ya
Tajikistan,Uchina na pakistan.
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Mwandishi
wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yenye
umaskini mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda ikachukua
majuma kadhaa kabla ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo.CHANZO BBC
SWAHILI
Post a Comment