Muda
wa wagonga nyundo: Kiungo wa West Ham, Stewart Downing, kulia,
akishangilia bao lake na Mark Noble baada ya kutia kambani mpira dhidi
ya Tottenham Hotspur'
WEST
Ham imeshinda mechi ya tatu mfululizo msimu huu baada ya kuifumua
Tottenham Hospur mabao 2-0 katika mchezo wa mapema wa lgi kuu soka
nchini England.
Bao la kujifunga la Harry Kane na goli la adhabu ndogo kupitia kwa Stewart Downing limetosha kumpa ushindi mnono Sam Allardyce.
Gundu kwa Spurs ilianza dakika ya 25 kipindi cha kwanza baada ya Younes Kaboul kuoneshwa kadi nyekundu.
Dakika
10 baadaye, West Ham waliandika bao baada ya Andy Carroll kupiga kichwa
mpira wa kona uliochongwa na Mark Noble, lakini mpira ulitua kichwani
mwa mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane na mpira kumchengua kipa Hugo
Lloris na kuzama nyavuni.
Wakiwa
10 uwanjani, Spurs walijitahidi kusaka bao la kusawazisha, lakini
walivurugwa zaidi baada ya goli la pili la adhabu ndogo iliyochongwa na
Sterwart Downing.
West Ham walishambulia zaidi kipindi cha pili lakini hawakuongeza bao lolote kutokana na uimara wa kipa Lloris.
Kaambulia manyoya: Hugo Lloris akishindwa kuokoa mpira wa adhabu wa Downing
Andy Carroll akiwapungia mkono mashabiki wao baada ya West Ham kuandika bao la kuongoza kutokana na Harry Kane kujifunga
Kazi bure: Kipa wa Spurs Hugo Lloris na Gylfi Sigurdsson wakishindwa kuzuia mpira wa kichwa cha Kane
Nje: Mwamuzi Phil Dowd alimzawadia kadi nyekundu Kaboul, kushoto, huku nahodha wa Spurs Michael Dawson akilalamika.
Kikosi
cha West Ham: Adrian, Demel, Tomkins, Reid, McCartney, Noble, Taylor,
Diame, Nolan (Jarvis 88), Downing, Carroll (Cole 84).
Kikosi
cha Tottenham: Lloris, Naughton, Dawson, Kaboul, Rose, Lennon, Paulinho
(Sandro 65), Sigurdsson (Soldado 66), Eriksen, Adebayor, Kane
(Chiriches 28)
Post a Comment