Nguzo hii ina zaidi ya Mwezi mmoja ikiwa ndani ya nyumba ya mtu na hatari zaidi kwa sababu imelalia katika miti mibichi
Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti
Nguzo
ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la
Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo iliyo haribika
Hizi ni nyaya za umeme ambazo zimepita Chini ,pia ni hatari kwa watembea kwa miguu
*****
Kutokana
na mvua zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo mvua
hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundo mbinu mbalimbali .
Uharibifu
mkubwa na wahatari ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika na baadhi
ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa
wananchi.
Katika
eneo la Mlalakuwa mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa
unaelekea kawe pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika kabisa na
nyingine mbili zimelegea katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika
la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua
hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya
mti ulio pandwa pembeni mti huo si mkavu ni mbichi.
Je
shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu
vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili
sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi
,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?
Tunaomba muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapobaadae kwani ni hatari sana. Picha na Dar es salaam yetu Blog
Post a Comment