WINGA hatari wa Asernal, Theo Walcott anaamini kushinda taji la FA itakuwa kichocheo cha kushinda mataji mengi misimu ijayo.
Imepita miaka 9 sasa tangu Arsene
Wenger abebe `ndoo` ambapo kwa mara ya mwisho aliifunga Manchester
United kwa penati na kutwaa kombe la FA mwaka 2005.
Asernal wanayo fursa ya kufuta
ukame huu watakapokutana na Hull City katika mechi ya fainali ya FA mei
17 mwaka huu na Walcott anaamini wakishinda italeta upepo mpya Emirates.
“Kama tutashinda FA kwa
kuzingatia jinsi tunavyocheza sasa, wachezaji watakuwa na hamu ya
makombe zaidi. Walcott ameiambia Tovuti ya Asernal.
“Nadhani kombe la kwanza ni muhimu- ukishinda, utashinda mengi zaidi. Nina uhakika na hilo”.
“Itakuwa heshima kwa bosi wetu kushinda kombe tena”.
“Ametuami kwa miaka yote. Kama hatuchezi vizuri, siku zote ananyoshewa vidole hata kama ni makosa yetu”.
Asernal walianza kwa kasi msimu
huu na kutabiriwa kushinda taji la ligi kuu nchini England, lakini
waliyeyuka mithiri ya barafu na kuziachia Chelsea, Man City na Liverpool
ziendelee kupambana.
Walcott hajapangwa tangu mwezi
januari mwaka huu kutokana na majeruhi, lakini anaamini kurejea kwa
Aaron Ramsey, Jack Wilshere na Mesut Ozil kutaweza kutimiza ndoto zao
kuelekea fainali ya FA.
Aliongeza: “Kuwakosa Aaron,
Mesut, na Jack, kocha wetu alisema itakuwa ngumu kuzoeana. Ukiwatoa
wachezaji hao watatu kwenye kikosi, timu itaathirika”.
“Ilikuwa huzuni kwa kila mtu kuwapoteza wachezaji hawa kwa wakati mmoja, lakini lazima mjitahidi kukaza”.
Post a Comment