KOCHA
wa Chelsea, Mreno, Jose Mourinho amelaumu kuwa majeruhi katika kikosi
chake na uchovu kwa wachezaji imekuwa sababu ya kupoteze mechi dhidi ya
Atletico Madrid.
The Blues walitandikwa mabao 3-1
Stamford Bridge usiku wa jana na kutolewa katika hatua ya nusu fainali
ya UEFA kwa wastani wa mabao 3-1 kufuatia suluhu ya bila kufungwa
Vicente Calderon.
Mourinho amewasifu wachezaji wake
kwa kupigana kwasababu kwa muda wote walikuwa wanajitahidi kujiweka
fiti kwa ajili ya mechi, lakini kulikuwa na matatizo mengi kwa Chelsea.
“Nilisema jumanne, wachezaji wangu walikuwa tayari na walitaka kuwa tayari kwasababu walitaka kucheza”.
“Walitaka kusaidia, kwasababu
walijua kuwa tuko karibu na fainali, lakini wakati huo huo tulikuwa na
matatizo mengi”. Mourinho aliwaambia waandishi wa habari .
“Kwa hiyo kila mchezaji alijituma
kadri awezavyo na Eto`o hakuwepo muda mwingi wa mazoezi. Oscar alikuwa
benchi na alikuwa majeruhi”.
“Tulikuwa na matatizo mengi,
lakini wachezaji walicheza kwa kujituma na nina furaha nao. Wameenda
nyumbani na huzuni, lakini na nyuso za furaha”.
“Walifanya kazi yao, wamepoteza mechi, lakini wamepoteza dhidi ya timu bora”. Alisema Mourinho.
Post a Comment