Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LOWASSA ASTAAJABISHWA NA DEO FILIKUNJOMBE


Lowassa akisalimiana na viongozi wa kata za Ludewa walipotembelea bunge juzi

Lowassa akisalimiana na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Honolatus Mgaya juzi mjini Dodoma








Lowassa akisalimiana na mjumbe Elisha ambae ni dereva wa CCM Ludewa





WAZIRI mkuu wa zamani Edward Lowassa na wabunge mbali mbali wamempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali za kuwakomboa wana Ludewa .

Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli alitoa pongezi hizo mjini Dodoma juzi nje ya ukumbi wa bunge wakati akisalimiana na viongozi wa CCm ngazi ya kata zaidi ya 92 waliofika bungeni kushuhudia shughuli za bunge kwa mwaliko wa mbunge Filikunjombe.

" Wana Ludewa mna kila sababu ya kujivunia kwa kuwa na mbunge mchapa kazi ninyi mnamwita Jembe ila mimi namwona zaidi ya jembe ni katapila na hamkokosea kumchagua nawaombeni mtunzeni mbunge wenu na epukeni na michepuko kwani ni mbunge makini na anayependa kuwatumikia"alisema Lowassa

Mbunge wa jimbo la mbinga Magharibi kepten John Komba amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kutokana na jitihada mbali mbali anazoendelea kuzifanya katika kuwatumikia wana Ludewa.



Komba ametoa pongezi hizo juzi wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wajumbe 92 kutoka jimbo la Ludewa ambao ni wenyeviti kata na makatibu kata kutoka kata zote 25 za jimbo la Ludewa na viongozi wa wilaya ambao wapo katika ziara ya siku nne mjini Dodoma na Dar es Salaam .



Alisema kuwa jembo kama Filikunjombe katika historia ya jimbo la Ludewa ni aliyepata kuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Holace Kolimba na baada ya hapo mbunge mchapakazi ni Filikunjombe .



“Nasema mmlea Deo Filikunjombe ni mbunge atakayefanya makubwa jimbo la Ludewa kutokanana jitihada zako za kimaendeleo na kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la Ludewa ….nataka kuwaambieni leo viongozi ambao mpo hapa Filikunjombe kwangu mimi amekuwa msaada mkubwa sana”



Hata hivyo alisema kuwa jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na Filikunjombe pamoja na wabunge wengine wa mkoa wa Ruvuma ambao wanazunguka ziwa nyasa kutokana na adha kubwa ya usafiri ila kwa sasa kero ya usafiri ikiwemo ile ya mlima kandamija



Pia amewaonya wana Ludewa kuacha kutafuta mbunge kama ndugu yao na badala yake kumtafuta mbunge wa ajili ya kuwapelekea maendeleo kama ilivyo kwa mbunge huyo ambaye amekuwa ni mwabikaji mzuri kwa wananchi.

“Mkimuacha Deo Filikunjombe Ludewa mmekosa mambo na mmekosa maendeleo katika jimbo hilo hivyo ni lazima kuendelea kumtunza ili azidi kuwatumikia zaidi”



Komba alisema kuwa wilaya ya Ludewa mbali ya kuwa na utajiri mkubwa madini ila wabunge wote waliopita walikuwa wakizungumzia suala hilo bila kuonyesha jitihada ila toka ameingia Filikunjombe madini hayo yameanza kushughulikiwa .



Alisema kuwa kwa sasa wananchi wa Mwambao kilio chao kikubwa ni meli na kuwa tayari wabunge wote wa Mwambao wameungana kuona wanapigania upatikanaji wa meli hiyo ili kutatua kero ya usafiri ziwa Nyasa .



“Mwisho nasema endeleeni kumpatia ubunge Deo Filikunjombe msibadilishe wabunge kama gauni…wenzetu wa kaskazini wanatushinda katika hilo mfano Msuya aliacha ubunge baada ya kusema mwenyewe sasa basi baada ya kufikisha maendeleo makubwa ikiwa ni pamoja na kufikisha umeme hadi chooni ….ila sisi baada ya kipindi kimoja tunasema aliyevivyo(amekula hivyo hivyo)”alionya Komba .



Huku kwa upande wake , Mbunge wa Mbinga Mashariki Gaudence Cassian Kayombo alisema kuwa mbali ya wana Ludewa kumuona mbunge wao ni jembe ila kwake na wabunge wengine na kusini wamekuwa wakimuona ni mkombozi wa maendeleo mikoa ya kusini.



Kayombo pia amewaonya wana Ludewa kuachana na tabia ya kubadili wabunge kama nguo na kuwa iwapo mbunge wao asingekuwa mchapakazi ni wazi harufu ya upinzani ingeanza kujitokeza katika jimbo hilo ambalo limeendelea kuwa ni tishio hata kwa vyama vya upinzani .



Kwani alisema jitihada za wana Ludewa kujaribu kwa sasa zimefika kikomo baada ya kumpata mbunge huyo ambae ni mchapakazi mzuri na kuwa ni vema wana Ludewa hawana haja ya kuendekeza uchoyo .



“Kitu ambacho kitaendelea kuiweka CCM madarakani ni umoja na mshikamano na bila umoja na mshikamano hakuna chama na hakuna mbunge ndani ya CCM”



Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Hilda Ngowi mbali ya kumpongeza mbunge Filikunjombe kwa maendeleo bado alisema kuwa mbunge huyo ameleta ngunzo kubwa bungeni kwa kuvunja rekodi ya kukaribisha wageni wengi zaidi bungeni tukio ambalo ni la kwanza kwa mbunge kuleta wabunge wengi kiasi hicho bungeni.

Huku mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akisema kuwa anatamani sana kufika Ludewa ili kumuunga mkono mbunge Filikunjombe ambae amekuwa ni ngunzo katika bunge kwa utendaji kazi na kutetea maslahi ya wananchi wake na Taifa.

Mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugola alisema kuwa kamwe katika ubunge wake hatakuja kumsahau mbunge Filikunjombe na kudai kuwa lazima viongozi wa kata na wanachi wa jimbo la Ludewa kuachana na michepuko kwa kutazama huku na kule badala yake kutulia njia kuu kwa maana ya kuendelea kufanya kazi na Filikunjombe.



Wakati Filikunjombe akidai kuwa wito ambao wajumbe hao wameonyesha ni wito mzuri zaidi na kuwa hilo ni deni kwake na malipo yake ni kuwafikishia maendeleo jimboni.


Kwani alisema kuwa kamwe hatawaangusha katika utendaji kazi wake na kuwa ni lazima aendelee kufanya kazi kwa moyo zaidi ili kuwapa imani wananchi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top