Watoto pacha waliotenganishwa, Eliud na Elikana watafanyiwa upasuaji mwingine ili kuwatengenezea njia ya mkojo ya kudumu.
Pacha hao
walizaliwa wakiwa na njia moja ya haja kubwa na ndogo, hali iliyowapa
wakati mgumu madaktari wakati wa operesheni ya kuwatenganisha.
Akizungumzia
hali ya Eliud baada ya kufanyiwa upasuaji wa kurejesha utumbo wake
ambao ulijitokeza, Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Watoto, Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Zaituni Bokhary alisema hali yake inazidi
kuimarika.
Alisema
pia kuwa, wiki hii watamfanyia upasuaji Elikana ili kuirudisha ndani
sehemu ndogo ya utumbo wake ambayo nayo ilikuwa nje. Baada ya kukamilika
kwa upasuaji huo, tatizo la njia ya haja kubwa itakuwa imetatuliwa kama
ilivyo kwa mwenzake.
Dk
Bokhari alisema baada ya kupona, watoto hao watafanyiwa upasuaji
mwingine ili kurekebisha njia zao za mkojo na kuzifanya za kudumu.
Alisema kwa sasa wanatumia njia za haja ndogo walizotengenezewa kwa
ajili ya kutumika kwa muda mfupi.
Alisema
kabla ya upasuaji wa kuwatenganisha, pacha hao walikuwa na njia moja ya
mkojo pamoja na uume mmoja. Hata hivyo, njia ya mkojo ilikuwa chini ya
korodani badala ya kupita katika uume.
“Baada ya
miezi mitatu, watafanyiwa upasuaji mwingine ili kuziba tundu la njia ya
mkojo na kuwatengenezea njia nyingine ya kawaida,” alisema na kuongeza
kuwa tatizo hilo linawakumba hata watoto wengine nchini.
Baba wa
watoto hao, Eric Mwakyusa alisema Eliud anaonekana mwenye furaha baada
ya operesheni hiyo tofauti na alivyokuwa awali utumbo wake ulipokuwa
umejitokeza nje.
Pacha hao
walipelekwa India mwaka jana kwa ajili ya upasuaji mkubwa wa
kuwatenganisha ambao ulifanikiwa. Hata hivyo, sehemu ya utumbo mpana wa
Eliud ilijitokeza nje kabla ya kufanyiwa upasuaji mdogo hivi karibun
Post a Comment