Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AMOS MAKALA ACHARUKA ..... GAZETI LA UHURU LAPEWA SIKU 7 KUMUOMBA MSAMAHA WAZIRI, LA SIVYO........!!!!!

 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNmJnhfBLoKqSPYspE_mXVbKMPQ5zmUhrkx-770JSuRMo5Bj3V_OOfOVVFcb2Z06tDM7IdRBSrl-5EIoq7fSdBKSPJY8wzSJksYAUD_lmvzAwrZ3twxcFHfKLR6n2Lq4-PqT62FyBhTXk/s1600/download+(2).jpg 
Nimesoma habari gazeti la UHURU la leo tarehe 9 Julai,2014 lenye kichwa cha habari TRA YAZUIA GARI LA NAIBU WAZIRI.Adaiwa kukwepa kulipa kodi kwa miaka miwili kodi ya leseni ya barabara.Nachukua fursa hii kukanusha habari hizo kuwa ni za uongo zenye hila na mwelekeo wa kisiasa kwa aliyeandika kwa makusudi kwa lengo la kunichafua na kunishushia heshima yangu.Habari iliyoandikwa imejaa uzushi,hila na upungufu mkubwa wa kimaadili ya kiuandishi wa habari.

NAOMBA uma wa watanzania kujua yafuatayo:


1.MIMI AMOS GABRIEL MAKALLA si mmiliki wa gari tajwa noT534BFP

2.Kodi inayodaiwa sh 662,500(laki sita sitini na mbili elfu mia tano tu) kwa mujibu wa taarifa za mwenye gari mpaka habari hii inaandikwa zilikwisha kulipwa.

HIVYO BASI,kutokana na ukweli huo habari hii ililenga kunichafua kwa makusudi na ina chembechembe za kisiasa na hila dhidi yangu na  kwa uzito huo

1.Nimemwagiza mwanasheria wangu AMICUS Advocates kuwaandikia gazeti la UHURU,MHARIRI na MWANDISHI WA HABARI HII kuniomba radhi  NDANI YA siku SABA kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti  kwa matoleo MATATU MFULULIZO

2.Kinyume na hilo nawashitaki gazeti, mchapishaji, mhariri na mwandishi na kunipa fidia Tshs 1,000,000,000 (Tshs Bilioni moja tu)

NARUDIA kusisitiza kuwa uandishi wa aina hii si tu unatia mashaka taaluma ya mwandishi aliyeandika bali pia ametumia kalamu yake kufanya siasa za maji taka na ili ukweli ujulikane nawakaribisha mahakamani ...

asanteni

AMOS G MAKALLA
Mbunge mvomero na naibu waziri maji
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top