Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

40 YA TYSON MAMA YAKE AUGUA GHAFLA

 


Na Mwandishi Wetu
WAKATI jana, Julai 9, 2014 George Otieno Okumu ‘Tyson ametimiza siku 40 tangu kifo chake kilichotokea kwa ajali mbaya ya gari mkoani Dodoma, mama mzazi wa marehemu, Gladys Okumu ameripotiwa kuugua ghafla nchini Kenya anakoishi.
Marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson' enzi za uhai wake.
Mama Tyosn amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan University iliyopo jijini Nairobi nchini humo kwa kile kilichoelezwa na madaktari kwamba anasumbuliwa na presha ya kushuka. Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, ndugu wa karibu wa marehemu Tyson ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa sababu si msemaji wa familia, alisema tangu kifo cha mwanaye, mama huyo amekuwa akisumbuliwa na presha hiyo.
“Kifupi tangu George (Tyson) amefariki dunia mama hayuko vizuri kiafya. Juzi (Jumapili) alizidiwa akakimbizwa Hospitali ya Aga Khan na kulazwa.
“Kikubwa ambacho naamini kimekuwa kikimsababishia tatizo hilo ni kitendo cha kutopewa undani wa ajali iliyomuua Tyson.
Mama mzazi wa marehemu Tyson , Gladys Okumu (kulia) akimlilia mwanaye.
“Yaani alichoambiwa yeye ni kuwa, mwanaye amefariki kwa ajali ya gari. Sasa ilikuwaje, wapi, walikuwa wangapi, wangapi walipona, walikuwa wakitokea wapi kwenda wapi? Hajawahi kuambiwa,” alisema ndugu huyo.
Naye ndugu mwingine wa marehemu Tyson aliye jijini Nairobi alipozungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu, alikiri mama huyo kusumbuliwa na presha na kulazwa.
Tyson alifariki dunia Mei 30, 2014 katika ajali mbaya ya gari aina ya Toyota Noah iliyotokea eneo la Gairo akitoka Dodoma mjini na wenzake watano ambao walinusurika kifo kwa kujeruhiwa na kutibiwa. Alizikwa Juni 14, mwaka huu kwenye Kijiji cha Siaya, Kisumu, Kenya.
GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top