Diwani aliyesimama Bi. Twilumba Wapalila enzi za uhai wake akiendelea na majukumu yake kama mwakilishi wa wananchi.
********
Diwani wa kata ya Lupembe wilayani Njombe Bi Twilumba Wapalila,
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam alikokuwa
akipata matibabu katika hospitali ya Muhimbili.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika
zilizopatikana kutoka kwa viongozi kabla ya kuanza kwa kikao cha
baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wamesema kuwa
hii leo watalazimika kufupisha kikao kutokana na msiba huo.
Aidha Baadhi ya wajumbe hao licha
ya kuonekana kuwa na simanzi lakini pia wamebainisha kuwa marehemu
alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Msiba huu ni wa pili kwa tarafa ya
Lupembe na wa tatu kwa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe kufuatia
siku chache zilizopita aliyekuwa diwani wa kata ya mfiliga kufariki
ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutokea kwa msiba wa aliyekuwa mwenyekiti
wa chama Hicho Marehemu Adam Msigwa.
Na James Festo via Hfesto blog
Post a Comment