MKONGWE wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ anasakwa na polisi kwa RB namba OB/RB/11650/2014 KUTISHIA KUUA mganga wa jadi Mery Kapalisya ambaye inadaiwa alikuwa akiishi naye kama mkewe.
Akisimulia mkasa mzima, Mery alisema
Dudubaya alitishia kumuua mara baada ya kumfukuza katika nyumba
waliyokuwa wakiishi pamoja maeneo ya Tandale, jijini Dar.
“Mimi na Dudu (Dudubaya) tulikutana baada ya kukutanishwa na Mabovu
(msanii) ndipo tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi baada ya kuniomba niwe
naye na kunieleza matatizo yake.
“Kwa sababu nilimpenda niliamua
kumkubalia na kuanza naye maisha ambapo tulikuwa tukilala katika baa
yangu nyumbani kwa akina Mabovu.
“Tukiwa ndani ya uhusiano, Dudubaya alianza kunibembeleza kwamba baa
ile tuipe jina la Mamba ikiwa ni chata yake, kwa sababu nilimpenda
niliamua kumkubalia lakini nilimwambia aongeze herufi nyingine mbili
ambazo zitamaanisha na mimi nahusika, tukakubaliana,” alisema Mery na
kuongeza:
“Baada ya baa kubadilishwa jina, matatizo yakaanza taratibu kwani
walijaa wasanii wa kila aina, baa ikaanza kuwa na sifa mbaya mpaka
wateja wote wakaondoka wale waliokuwa wanajiheshimu.”
Mery alisema
alikuwa akimuonya Dudubaya juu ya tabia za kumsaliti na kulala na
wanawake ndani ya nyumba pale anapokuwa amesafiri kwenda kwenye mambo ya
kitabibu lakini alikuwa hasikii.
“Baada ya kunifukuza nyumbani, amenitumia maneno mazito sana ambayo
siwezi kusimulia kiukweli lakini ninao ushahidi wa SMS,” alisema Mery
alipokuwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Wakati Mery alipokuwa
kituoni hapo, polisi walimpigia simu Dudubaya, akasikiliza maelezo ya
polisi kisha akakata simu na alipopigiwa tena, hakupokea.
Chanzo: Gpl
Chanzo: Gpl
Post a Comment