Shirikisho la Kandanda la Dunia, FIFA, limeionya Nigeria kwamba
itatolewa katika kandanda ya kimataifa iwapo serikali haitalirejesha
tena shirika la kandanda la Nigeria, Nigerian Football Federation,
ifikapo Jumaane juma lijalo.
Siku ya
Alkhamisi serikali iliifuta Nigerian Football Federation na Ijumaa rais
wa shirika hilo alikamatwa baada ya kurudi kutoka Kombe la Dunia.
Nigeria ilishindwa kwenye mechi na Ufaransa na hivo kukosa kuingia katika robo-fainali.
FIFA imesema imetiwa wasi-wasi na hatua ya serikali ya Nigeria dhidi ya chama cha kandanda cha nchi hiyo.
Kanuni za FIFA zinaeleza wazi kuwa wanachama wake lazima waruhusiwe kufanya kazi yao bila ya kuingiliwa kati na serikali.
Wakuu wa
Nigeria wamekifuta chama cha kandanda cha taifa na piya kumkamata rais
wa chama; na waziri wa michezo amemteua mkurugenzi wake kuongoza chama
hicho.
Haijulikani sababu ya serikali ya Nigeria kufanya hivyo.
Lakini iwapo serikali haitabadili uamuzi wake basi Nigeria haitaweza kushiriki katika mechi za kimataifa, mazoezi na kadhalika.(A.I).
Post a Comment