Filamu ya Scola ya mwigizaji Aunt Ezekiel imezuiwa kuingia
sokoni na bodi ya Filamu Tanzania kutokana kuwa na “scene” zinasemekana
kuwa kinyume na maadili ya Tanzania.
Filamu hii imegundulika kuwa ina matatizo hayo baada ya
muigizaji huyo kuipeleka kwenye bodi hiyo ili ikaguliwe kabla ya kuingia
sokoni
Kupitia rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa
rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika
mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.
“Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa Aunt.
Alipotafutwa Aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.
Mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya Sister Mary baada ya kuridhishwa na madai ya Kanisa Katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha Ukatoliki.
Habari kwa hisani ya Global Publishers
Post a Comment