Stori: Paparazi Wetu
SOO! Mtangazaji
anayedili zaidi na mambo ya haki za wanawake Bongo, Joyce Kiria
amenagwa na watu mbalimbali mitandaoni kwa kile kinachoonekana kuingilia
sakata la mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel
Mbasha, akionekana zaidi kumtetea Flora.
Mmoja wa watoa maoni katika mtandao wake
aliandika: “Joyce acha kujidhalilisha, huoni kama unapoteza utu wako?
Naanza kuamini kuwa na wewe ni miongoni mwa wasioheshimu ndoa zao
kutokana na kuwashauri wenzako upumbavu!
“Kwa mantiki hiyo hustahili hata kuwepo
kwenye Kipindi cha Wanawake Live, ikiwa unatetea upumbavu. Acha
kuingilia mambo yaliyopo mahakamani, utapoteza mashabiki wako bure.”
Licha ya kunangwa kwa maneno makali mara
kwa mara, Joyce ameendelea kuandika kila wakati kuhusiana na ishu hiyo,
akionyesha hisia zake waziwazi kuwa yupo upande wa Flora jambo ambalo
limepingwa vikali na wachangiaji walio wengi, wakimtaka asijadili suala
lililopo mahakamani.
Post a Comment