Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe
Jacinto Nyusi kwenye hotel ya Golden Tulip ambapo alikuwa na mazungumzo
naye .
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria
akisalimiana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo
Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, kabla ya kuanza mazungumzo kwenye
hoteli ya Golden Tulip.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya
Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akijibu baadhi ya maswali ya
waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu mahusiano yao na CCM pamoja
na namna Demokrasia inavyoendeshwa nchini Msumbiji,Mheshimiwa Nyusi
alisema mahusiano yao na CCM ni mazuri na ya kihistoria Tangia wakati wa
mapambano ya Ukombozi,alipoulizwa kuhusu uwezo wake wa kuongea
Kiswahili vizuri alisema wakati wa mapambano ya Ukombozi aliwahi ishi
Tunduru na Nachingwea nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif
Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa
wengine wa Chama Cha Mapinduzi kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa
Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe
Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa Nyerere,Golden Tulip
Hotel.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif
Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye meza ya
mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha
Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa
Nyerere,Golden Tulip Hotel.







Post a Comment