Mahamudu Madenge |
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga |
Baadhi ya mabalozi wa mtaa wa kihesa wakiwa katika semina hiyo |
********** |
Kiasi hicho cha fedha kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga kitatumika kutoa semina kwa mabalozi wa nyumba kumi kumi wa kata zote 16 za jimbo hilo.
Semina hizo zitakazowafikia mabalozi zaidi ya 1,900 katika kata zote 16
za jimbo hilo zilianza jana katika kata za Kihesa na Nduli.
Lengo
la semina hizi ni kuwakumbusha mabalozi wetu wajibu wao kwa chama na
wajibu wa chama kwao na kukijenga na kukiimarisha chama wakati
tukielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa,” alisMtenga ambaye pia ni Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa alisema chama hicho kina zaidi ya mabalozi 1,90
Alisema
mabalozi ni kitengo kinachotegemewa na chama hicho katika kuwaunganisha
wanachama wake na ngazi mbalimbali za chama na viongozi wake.
“Semina
hizi zimeanzia ngazi hii ya mabalozi, ni ngazi muhimu sana kwa
maendeleo ya chama chetu…..baada ya hapo tutaendelea na semina hizo kwa
wanachama na vingozi wa mashina, matawi, kata, umoja wa vijana na
wanawake, jumuiya ya wazazi na viongozi ngazi ya wilaya,” alisema
Akimshukuru na kumpongeza Madenge kwa kukiwezesha chama kufanya semina
hizo, Mtenga alisema ni kiongozi anayepaswa kuigwa kwasababu anajua na
anatekeleza majukumu yake ya kichama kwa kuzingatia nafasi aliyonayo.
Alisema
chama hicho kinaingia katika semina hizo kikiwa na mtaji wa wanachama
zaidi ya 26,000 huku kikiendelea kupokea wengine ambao kwa pamoja
wanatarajia kukiwezesha kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao
wa serikali za mitaa.
Akizungumzia
sababu ya kuchangia fedha hizo, Madenge alisema; “nilipochaguliwa kuwa
MNEC kuiwakilisha manispaa hii niliahidi kutumia nguvu zangu zote
kukijenga chama hiki.”
Alisema
asipofanya hivyo atakuwa awasaliti wanachama wa chama hicho,
waliomuamini na hatimaye kumpa jukumu zito katika chama hicho kwa
kumchagua kuwa muwakilishi wao katika vikao vya NEC.
“Napokwenda
kule na kwenye vikao vingine natakiwa niseme nimefanya kazi gani kwa
kutumia nafasi yangu hii katika kukijenga chama, naamini wana CCM wa
Manispaa ya Iringa hawakunichagua ili nitembee katika gari lenye bendera
bila kufanya kazi yoyote ya chama,” alisema.
Alisema kwa kutumia nafasi aliyonayo katika chama hicho ataendelea
kutafuta fedha ili semina kama hizo ziwafikie wanachama na viongozi
wengine wote wa jimbo hilo ambalo kwa mwaka wa nne sasa linaongozwa na
Mbunge kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji
Peter Msigwa.
Imechotwa: Mjengwablog
Post a Comment