

HATIMAYE
wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi wamekabidhi vifaa viwili vya kutunza
kumbukumbu (black boxes) vya ndege MH17 ya Malaysia iliyolipuliwa kwa
maofisa uchunguzi wa Malaysia huko Ukraine.
Makabidhiano
hayo yamefanyika ikiwa ni baada ya wito mbalimbali kutolewa kuhusu
maofisa wa uchunguzi kuruhusiwa kufanya uchunguzi wao eneo hilo la ajali
iliyouwa watu 298.
Waziri
Mkuu wa Malaysia, Najib Razak ameeleza kuwa vifaa hivyo vilikabidhiwa
mjini Donetsk jana baada ya mazungumzo ya muda mrefu na wapiganaji hao.
Post a Comment