ALIYEKUWA
Katibu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa TFF, Michael Wambura
ameishangaa kamati ya utendaji ya Simba ya kupeleka suala lake kwenye
mkutano mkuu, wakati sakata lake limeshamalizika na kamati ya rufaa ya
Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Julius Lugaziya.
Wambura
ameyasema hayo leo mchana alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari
alipowasilisha mada ya kuwatetea wanachama 69 waliosimamishwa kwa kosa
la kwenda mahakamani. Wambura amesema kitendo alichofanya Rais wa Simba Evans Aveva cha kuwasimamisha wanachama hao ni kuchochea migogoro.
Wambura akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam |
Wambura
alikwenda mbali zaidi kwa kusema hana haja ya kujadiliwa kwenye mkutano
wa Agosti 3, kwa kuwa alishasafishwa kwenye Kamati ya rufaa ya uchaguzi
iliyochini ya Mwenyekiti wake Julius Lugaziya.
“Mimi
nilishasafishwa kwenye kamati ya Lugaziya na ndio mana nilirudishwa
kwenye uchaguzi, na niliondolewa kwa kosa la kufanya kampeni tu hivyo
sina haja na mkutano wao,”alisema
Alisema
kwa mujibu wa Katiba ya Simba ibara ya 41(d) kuwanyima wanachama fursa
ya kujitetea na kusikilizwa kabda ya hatua ni uvunjifu wa haki za msingi
za binadamu. Kama zinavyoanishwa kwenye katiba ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Ibara ya 13(6)a pamoja na kanuni za nidhamu za FIFA ibara ya
94(1) na kanuni za adhabu za TFF Ibara ya 35 (1).
Wambura
ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa TFF
alisema wanachama waliokwenda mahakamani wana hoja za msingi hivyo
wasipuuzwe.
“Wangekuwa
hawana hoja hata mahakama kuu isingewapa haki ya kufungua shauri lao,
hivyo wasipuuzwe wapewe nafasi ya kusikilizwa,”alisema. Wambura
ambaye hii ni mara ya tano kuenguliwa kwenye uchaguzi alisema kitendo
alichofanya Aveva ni cha kidikteta na kitasababisha kuanzisha
mtafarakano upya ndani ya klabu hiyo.
Alisema
kwa mujibu wa katiba ya Simba Ibara ya 54 (3), uamuzi wowote wa
kufukuza wanachama lazima upigiwe kura za siri na wajumbe theluthi mbili
waunge mkono, hili japo sio rahisi kama wanavyorifikiria.
“Kuna
wakati Hassani Dalali alitaka kumpindua Mwina Kadugunda ila baadae
alikwama baada ya wanachama kukataa pendekezo hilo,”alisema.
Alisema uongozi wa Aveva hauwezi kupambana na wanachama zaidi ya 500, hawataweza vita hivi na lazima waingie kwenye migogoro.
Wambura aliishauri uongozi huo utafute suluhisho la mgogoro huo mapema kabda ya mgogoro huo haujawa mkubwa.
Alisema
japokuwa hawapewa barua rasmi na Rais wa Simba ila ushauri wake kama
wanachama atauwasilisha kwa maandishi kwenye uongozi huo.
“Haya yote nilioongea leo nitayawasilisha kwenye uongozi wa Simba ili wawe na kumbukumbu kama nimeyaongea,”alisema.
credit: Bin zubeiry
Post a Comment