Wasichana zaidi ya 200 wa Chibok waliotekwa na kundi la Boko Haram wanadaiwa kuwa katika hali mbaya na ya kutisha zaidi. Senator wa jimbo la Borno anasema hufanyiwa vitendo vya kinyama kupita maelezo.
Akifanya mahojiano na kituo cha runinga cha Sahara TV, Senator
Khalifa Ahmed Zanna wa Borno Central amesema amepata ripoti mpya kuwa
wasichana hao waliotekwa siku zaidi ya 70 zilizopita hubakwa na wafuasi
wa kundi hilo huku wakichukuliwa video ambayo baadae huoneshwa
hadharani.
Senator huyo ameeleza kuwa ingawa hakushuhudia video hiyo lakini mtu
aliyemsimulia matukio hayo alikuwa na video hiyo na alieleza kuwa
msichana akimaliza kubakwa hupiga magoti mbele ya mbakaji na kumuomba
amhurumie.
“Therefore the girl after being raped, she curled down to the
man, kneeling down and begging him to please be patient. So disturbing.
And although I didn’t see the video, the person narrated to me, he said
he had the video, and he was narrating to me, and look at the
situation.” Amesema Senator Khalifa.
Amesema mbali na wasichana hao waliotekwa, kundi hilo limewakamata wanawake zaidi ya 500 wanaokutwa barabarani au vijijini.
Mbali na tukio hilo la kinyama, amesema ripoti aliyopewa inaonesha
kuwa kundi hilo hivi sasa halina chakula cha kutosha hivyo linaingia
vijijini na kuwanyang’anya wanakijiji chakula walichonacho huku
wakifanya matukio ya kinyama.
Kufuatia matukio hayo wanakijiji wengi wamekimbia makazi yao na
kuhamia mijini bila kujua hatima yao huku wengine wakiingia kwenye nchi
za jirani.
Post a Comment