Makampuni
mbalimbali nchini Tanzania sasa hivi yameanza kuamka kwa nguvu
kuwatumia vizuri mastaa wa bongo kwenye kutangaza biashara zao ikiwemo
Fastjet, Airtel na Vodacom ambao walianza hii kitambo kidogo.
Kwenye list ya mwaka huu mwimbaji Linah nae yumo ambapo baada ya
kujituma kwa bidii kama kijana wa Kitanzania, kampuni ya NFZ anayofanya
nayo kazi imemzawadia gari hili aina ya Toyota Mark X.
Hii inaonekana kama baraka za kusaidia Wazazi manake miezi kadhaa
iliyopita Linah aliwazawadia Wazazi wake nyumba ambayo aliijenga kwa
ajili yake lakini baadae akabadili maamuzi na kuwazawadia wazazi.
Kwa sasa Linah ameshaanza ujenzi wa nyumba yake Mbezi jijini Dar es salaam.
Post a Comment