Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Scolari kuamua hatma yake baada ya kombe


Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema kuwa ataamua mustakabal wake baada ya kombe la dunia.
Scoalari aliyasema hayo baada ya aibu ya kutandikwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali Jumanne.
Vyombo vya habari vilimlimbikizia lawama kwa kichapo hicho lakini Scolari amesema kuwa atatua kauli yake baada ya mechi ya kuamua mshindi wa tatu dhidi ya Uholanzi siku ya Jumamosi.(P.T)
Kichapo hicho ndicho kilikuwa kibaya zaidi kuwahi kuipata Selecao tangu mwaka wa 1920 Brazil ilipolimwa 6-0 na Uruguay.

Kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 65 alikuwa ameiongoza Brazil mwaka wa 2002 lakini akondoka na kurejea mwaka wa 2012 kuiandaa timu hiyo kwa mashindano haya ya nyumbani.
Brazil walikuwa nyuma mabao 5-0 baada dakika 30 ya kipindi cha kwanza kabla ya kukamilisha mechi hiyo mabao 7-1.
Chanzo:BBC
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top