Baada
ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina na mzunguko mkubwa wa matumizi na
inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili mizunguko ni miezi
sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT) inatarajia kubadili noti hiyo na
kuifanya sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza kutumika July
2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo unaambiwa
hii sarafu ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya
miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule, yani ni imara kuliko noti.
Afisa
mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki Patrick Fata
ameongea na millardayo.com na kusema “Tunafanya hivi kwasababu noti ya
500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu
wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na watu
wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya
wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku’
Post a Comment