Watafiti wanasema kuwa wameweza kutafsiri maana ya ishara za mawasiliano zinazotumiwa na Sokwe wanaoishi msituni
Wanasayansi
hao waligundua hili kwa kuwafuatilia na kuwanasa kwa video Sokwe nchini
Uganda na kutathmini zaidi ya visa 5000 vya umuhimu wa mawasiliano
hayo.
Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la Bayolojia ya kisasa.
Daktari,
Catherine Hobaiter, aliyeongoza utafiti huo, anasema kuwa huu ndio
mfumo pekee wa kimataifa wa mawasiliano kuhusu wanyama kuwahi
kurekodiwa.
Ni binadamu pekee na Sokwe ambao wana mfumo wa mawasiliano ambapo walitumiana ujumbe kwa lengo fulani
Post a Comment