ijana wa B.O.B Micharazo, wakiongozwa na front runners, Mr Blue na Nyandu Tozi, wameachia video ya ngoma yao mpya iitwayo ‘Shut Up’ (Kimya).
Kwenye ngoma hiyo iliyotayarishwa na Marco Chali, rappers hao wanatoa onyo kali kuwanyamazisha wapinzani wao. Katika verse ya Mr Blue aliyefungua ngoma hiyo kuna mstari unaoelekea kumpiga dongo rais wa Masharobaro, Bob Junior.
“Helo Dar es Salaam mbona kimya jiji zima mbona limezizima/Hakuna cha Sharobaro wala ming’aro ya kuazima/ Mmebakiza uharo kumbe washenzi mlipima/Wabaya wetu mbona kimya, vipi wazima au nanyinyi mlipima,” anarap Kabayser.
Wengine waliochana kwenye ngoma hiyo ni Blood Gaza, Bobby MC, Cotton, Uswege na Beka Title aliyesimama kwenye chorus.
BOFYA PLAY
Post a Comment