Wanaohusika na ubadhirifu wa fedha za manunuzi ya Umma
watangazwe hadharani ili wafahamike na kuchukuliwa hatua stahil kwani
wamekuwa wakitumia fedha za umma kwa manufaa yao bila ya kujali.Changamoto
hiyo ilitolewa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salum wakati akifungua
warsha ya ppra kuhusu sheria ya ununuzi wa umma kwa wakurugenzi wa
bodi,wakuu wa taasisi na mashirika ya umma na wakala wa serikali jijini.Mkuya
alisema kumekuwepo na malalamiko mengi katika manunuzi ya umma huku
akifafanua kuwa takwimu zinaonyesha asilimia sabini ya bajeti ya kawaida
na asilimia mia moja ya bajeti ya maendeleo hutumika kufanya ununuzi
kiwango ambocho ni kikubwa sana hivyo ni muhimu kuweka udhibiti wa
ununuzi wa sekta hiyo.
Waziri
alisema upotevu au ubadhilifu unaoweza kujitokeza unaweza kuliingizia
taifa hasara kubwa kwani imeonekana asilimia kumi na tano hadi ishirini
la pato la taifa kutumika katika manunuzi ambapo kiwango hichi ni
kikubwa sana.
‘’Nawakumbusha
kuwa sekta ya manunuzi ya umma imekuwa ikiliingiza taifa kwenye deni
kubwa hivyo mnawajibu mkubwa wa kudhibiti manunuzi ili kuipunguzia
serekali mzigo kwani bila ya kufanya manunuzi yenye kukidhi kwa wakati
mtakuwa hamkuisaidia serekali bali mtakuwa mmefanya hiyana”alisema Mkuya
kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya ppra balozi dkt matern lumbanga
amesema warisha imeandaliwa kwaajili ya kuwaelimisha walengwa kuhusu
sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013
lengo likiwa ni kuboresha ununuzi wa umma
Lumbanga
alisema kuwa Tanzania imekuwa ikipoteza fedha nyingi kwenye manunuzi ya
umma hivyo mnao wajibu wa kukabiliana na changamoto hiyo huku
akitanabaisha kuwa ripoti ya utendaji wa ppra ya mwaka wa fedha 2012/13
imebainisha kwamba zaidi ya trillion nne zilitumiwa na taasisi za umma
265 kufanya manunuzi ya ukandarasi wa ujenzi ikiwemo vifaa na huduma
Huku
akisema kuwa maboresho yataendelea kuwepo kwenye sekta ya manunuzi
ilikuendana na viwango na sheria mpya ya manunuzi ya mwaka 2011 huku
akiwasihi wadau na wazabuni kufuata matakwa ya shria hiyo pia kuomba
ushauri badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari kutoa malalamiko
Post a Comment