Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza jambo na
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Ofisini kwake jijini
Dar es salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe wa
kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi na watendaji wa
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) iliyofanyika katika maeneo
mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Mkiti
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho
akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya
hali ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam mara baada
ya kukamilisha ziara ya siku nne mkoani Dar es salaam. Dkt. Fatma
ameeleza kuwa maabukizi yameendelea kupungua kutokana na juhudi kubwa
inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Wadau
mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya ziara ya watendaji wa
TACAIDS katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuangalia
hatua iliyofikiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU
katika jiji la Dar es salaam.
Viongozi
wa mkoa wa Dar es salaam na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi
wakichukua michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na wajumbe
waliohudhuria kikao cha majumuisho ya ziara ya viongozi wa TACAIDS
mkoani Dar es salaam.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akitoa mchango wake
kuhusu namna viongozi wanavyoweza kusaidia kupunguza vitendo hatarishi
vinavyochangia maabukizi mapya ya VVU katika maeneo wanayoyaongoza,
wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi na
watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) jijini Dar es
salaam.
…………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa-MAELEZO.
Dar es salaam.
Serikali
imewataka viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha
kuwa wanatoa kipaumbele na kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na
vitendo vyote vinavyochangia maambukizi mapya ya VVU katika maeneo
mbalimbali ya jiji hilo.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam, Saidi Meck Sadiki wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya
siku nne ya viongozi na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi
(TACAIDS) katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam.
Amesema
viongozi na watendaji wa jiji hilo ndio wenye dhamana na jukumu la
kusimamia na kuongoza mipango yote ya mapambano ya maambukizi mapya ya
VVU wakishirikiana na wananchi katika maeneo wanayoyaongoza na kufafanua
kuwa janga la Ukimwi lisipodhibitiwa katika ngazi zote litaendelea
kupoteza nguvu kazi na kuiongezea serikali mzigo wa kuwahudumia wagonjwa
wapya.
“Nawaagiza
viongozi wa manispaa zote tatu za mkoa wa Dar es salaam kulipa
kipaumbele kikubwa suala hili la mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwa
kuweka msukumo katika kutoa elimu ili tuweze kuokoa rasilimali zetu”
Amesema.
Amesema
serikali, vyombo vya habari na Taasisi zilizo kwenye mapambano dhidi ya
maambukizi ya VVU zimekuwa zikifanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya namna
ya kujikinga na janga hili na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa
wingi kupima afya zao kwa hiari ili kujua kiwango cha maambukizi ya
ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali ya jiji.
Ameeleza
kuwa licha ya mkoa kukabiliwa na changamoto mbalimbali umeendelea
kuchukua hatua za kupunguza maabukizi mapya ya VVU kwa kuweka msisitizo
katika utoaji wa elimu, kupiga marufuku ngoma hatarishi za usiku
zinazokesha, kutekeleza sheria mbalimbali kupitia jeshi la Polisi ambalo
huendesha operesheni mbalimbali za kuwakamata wananchi wanaovunja
sheria hususan waendesha biashara za madanguro,watumia madawa ya kulevya
na biashara ya ngono kwenye majumba ya starehe.
“Tunaendelea
kutoa elimu ya kujikinga na maabukizi mapya ya VVU ili kusaidia hata
operesheni mbalimbali tunazofanya katika jiji letu kuzaa matunda na
kuwafanya wale wote waliokuwa wakijihusisha na vitendo vinavyochangia
kueneza VVU kuachana navyo” Amesisitiza.
Aidha,
Bw. Meck Sadiki amegiza kupatiwa orodha ya maeneo yote ya jiji la Dar
es salaam ambayo yanaongoza kwa kuwa na vihatarishi vya VVU ili aweze
kuyafanyia kazi na kuwaomba wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kutoa
ushirikiano kwa kuunga mkono juhudi za serikali na kuwafichua
wanaoendesha vitendo vinavyochangia maambukizi hayo ili mamlaka husika
ziweze kuchukua hatua za kisheria.
Kwa
upande wake Mkiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt.
Fatma Mrisho akizungumza wakati wa majumuisho hayo amesema kuwa hali ya
maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam yameendelea
kupungua kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali.
“Ni
kweli hali ya maabukizi ya VVU kwa mkoa wa Dar es salaam imeendelea
kupungua mwaka hadi mwaka toka asilimia 10.9 mwaka 2004 hadi kufikia
asilimia 6.9 za mwaka 2012 jambo linalotufanya tuendelee kuongeza juhudi
zaidi ili tufikie malengo ya kitaifa na kimataifa ya kufikia sifuri
tatu”. Amesisitiza.
Amesema
ili kuhakikisha kuwa vita dhidi ya maambukizi mapya ya VVU inaendelea
kufanikiwa , Serikali inashirikiana na taasisi mbalimbali, Baraza na
mitandao ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini katika kutoa
elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na tatizo hilo.
Ameongeza
kuwa serikali inawathamini na inaendelea kuwajengea uwezo Wanaoishi na
Virusi vya Ukimwi waliojiunga katika Vikundi vya Kuweka Akiba na Mikopo
(VICOBA) katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na mwamko mkubwa wa
kujiletea maendeleo waliouonyesha.
Ametoa
wito kwa WAVIU kote nchini kuendelea kujiunga na mifuko mbalimbali
ukiwemo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili waweze kunufaika na
huduma za afya zinazotolewa kupitia mfuko huo.
Post a Comment