Jose
Serrano ni mtoto wa Ciudad Juarez kutoka nchini Mexico. Jose mwenye umri
wa miaka 11 sasa ana uvimbe ukubwa wa kutisha katika shingo yake na
amelazimika kuishi na uvimbe huo kwa maisha yake yote. Alipo zaliwa
uvimbe huo ulikua na ukubwa kiasi cha mpira mdogo, lakini umekua
ukiendelea kukua siku hadi siku na sasa kufikia kama inavyoonekana
kwenye picha.
Pamoja na
kwamba uvimbe huo umekua ukitishia maisha ya mtoto huyo tangu
ulupoonekana kwa mara ya kwanza, Madaktari wanasema hawakujua kama Jose
angeweza kuishi hata siku 1 baada ya kuonekana nao alipokua mchanga. Kwa
mujibu wa madaktari, uvimbe huo umezidi kua hatari zaidi sasa kwa
maisha ya mtoto Jose na unaweza ukaanza kuathiri mfumo mzima wa upumuaji
wa kijana huyu kwani umeanza kuingiliana na mfumo wa mapafu yake.
Hatahivyo
wazazi wa mtoto huyo wanamshukuru Mmishonari mmoja aliyekua akifanya
kazi katika shirika la kusaidia watoto yatima huko mjini Ciudad Juarez,
nchini Mexico. Mmishenari huyo alimkutanisha Jose na madaktari na
wataalam kutoka Hospitali ya watoto ya Chuo kikuu cha New Mexico, ambao
wanaamini wamepata ufumbuzi wa tatizo hilo. Na katika hali ya kushangaza
wanasema ufumbuzi huo ni vidonge aina ya VIAGRA!
Ingawa
sote tunajua Viagra ni nini na vinafanya kazi gani, kila mtu anajiuliza
inakuaje apewe mtoto wa miaka 11? Lakini madaktari wanasisitiza kua kazi
nyingine au uwezo mwingine wa vidonge hivyo ambao haujulikani na wengi
ni kutibu au kunyong’onyeza uvimbe kama wa mtoto Jose.
Pia
Mmishenari ameweza kuanzisha mfuko wa kujitolea kuchangia ili kumwezesha
mtoto huyo kulipia matibabu hayo, ambayo yanagharimu kiasi cha Dola
2,000 kwa wiki (sawa na Tsh. Mil 3.2) kwa ajili ya Madawa na Dola
125,000 (sawa na Tsh. Mil 200) kwajili ya Upasuaji na Matibabu. Pesa
hiyo yote imefanikiwa kukusanywa kupitia michango kutoka Hospitalini,
Kanisani na watu mbalimbali. Pia kampuni ya Pfizer ambayo inatengeneza
vidonge wamejitolea kulipia gharama zote za vidonge Hivyo.
Jose
mwenyewe anashangazwa na kufurahishwa na hayo na anatumaini kua matibabu
hayo yatamwezesha kuishi maisha ya kawaida. “Kama madaktari
watafanikiwa kunitibu, nitafurahi sana. Nitakua na furaha na nitaweza
kuishi maisha ya furaha na kufanya kilakitu ninachotaka.” Alisema mtoto
Jose kwa hisia kali.
Share habari hii, kisha andika “AMEN” kwenye comment kama unamtakia mafanikio mtoto Jose katika matibabu yake.
Post a Comment