Siku mbili zilizopita kumekuwa na taarifa mitaani kuwa mwimbaji ambaye pia ni producer wa Sharobaro Records, Bob Junior alifanyiwa fujo na mwanaume mmoja anaedaiwa kuwa mume wa msichana aliyekuwa anafanya naye video.
Taarifa hizo zilieleza kuwa tukio hilo lilifanyika maeneo ya Mlimani City wakati Bob Junior alipokuwa akishuti vipande vya wimbo wake wa ‘Bolingo’ huku msichana huyo akijiachia mbele ya lens.
Ghafla mumewe akatokea na kuzua tafrani, video ya wimbo ikageuka kuwa ya ndondi na mwisho wa siku mwimbaji huyo alilazimika kukimbia kupisha shari.
Tovuti ya Times Fm imeongea na Bob Junior kuhusu tetesi hizo ambapo yeye amekiri kutokea kwa fujo hiyo lakini amekanusha kuhusu suala la kufanya video na msichana huyo ingawa alikuwa na directors wake na vifaa.
“Hapana, naona watu wanakuwa kama wambea. Mimi nilikuwa nimekaa pale Mlimani City tunapiga story niko na mwanamke wangu. Rafiki yangu mwingine alikuwa kaka na mwanamke mwingine, sasa sijui kama ni mke wa mtu au nini, ndio ikatokea vurugu lakini huyo mwanamke aliyefanyiwa vurugu mimi simfahamu.” Ameeleza Bob Junior.
“Tulikuwa tumekaa tu tunaenjoy tunapiga story, tunakula…mimi sijui kama ni mwanamke wake au ni mke wake. Amemfanyia vurugu, amemvuta nywele. Wamezinguana kidogo lakini sifahamu kama ni mke wake au ni mchumba wake ila najua ni mtu ambaye ana uhusiano nae.” Ameongeza.
Akizungumzia kuhusu taarifa kuwa alitoka nduki na kumuacha rafiki yake akifanyiwa fujo, Bob ameeleza kuwa aliondoka kupisha shari na sio kukimbia kama ilivyotafsiriwa.
“Hapana siwezi kukimbia siwezi kukimbia. Tanzania ni nchi yenye amani kwa nini nikimbie kuna vita gani jamani hapo. Mimi nilichukua vitu vyangu na vijana wangu na team Sharobaro wangu, nikaondoka taratibu nikachukua gari langu nikaondoka. Unapoona mtafaruku hupaswi kukaa kuendelea kuangalia jambo. Unapaswa kupisha uliache jambo liendelee.”
SOURCE: http://www.timesfm.co.tz
Post a Comment