Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kitawachukulia hatua
kali wabunge wake iliyowaita kuwa ni wasaliti kwa kupuuza maagizo ya
chama na kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba
vinavyoendelea mjini Dodoma.
Mkuu
wa kurugenzi ya sheria ya CHADEMA na msemaji wa kambi rasmi ya upinzani
Bungeni Tundu Lissu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam muda mfupi
baada ya chama hicho kutoa taarifa ya kuwepo njama za kutaka
kukidhoofisha chama hicho.
Kwa mujibu wa Lissu, mamlaka ya nidhamu kwa wanachama wenye hadhi ya ubunge ni kamati kuu, chombo ambacho amesema ndiyo kilichotoa maagizo ya kwamba wajumbe wote wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kutoka CHADEMA wasihudhurie vikao vya bunge maalumu la Katiba.

Post a Comment