Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Diamond na Dabo watajwa kuwania tuzo za 'IRAWMA', Marekani



Wasanii wa Tanzania, Diamond Platinumz na Dabo (wa Dancehall) wametajwa kuwania tuzo za IRAMWA (International Reggae and World Music Awards), Marekani.
Wimbo wa MdogoMdogo wa Diamond umemuwezesha kutajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha The Best African Song/Entertainer akichuana na Davido (Aye), Awilo Longomba (Bendeke), Willy Paul Msafi (Tam Tam), Eddy Kenzo (Sittya Loss), na Bracket (Mama Afrika).


Naye msanii wa dancehall, Dabo ametajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best New Entertainer.

Upigaji kura tayari umeshafunguliwa na tuzo hizo zitatolewa October 4 nchini Marekani.
Wapigie kura wasanii hawa wa nyumbani ili kuwawezesha kuleta ushindi nyumbani. Ingia www.irawma.com na uchague vipengele wanavyoshindania.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top