Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akipokea ufunguo
wa moja kati ya magari kutoka kwa mwakilishi wa shirika la GLRA nchini
Burchard Rwamtoga (kushoto) ikiwa ni ishara ya kukabidhi msaada wa gari 4
na pikipiki 20 vyenye thamani ya Tsh. Milioni 261 jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi akiwasha moja kati ya
magari manne aliyoyapokea kutoka kwa mwakilishi wa shirika la GLRA la
Ujerumani nchini Burchard Rwamtoga jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
wa shirika la GLRA nchini Burchard Rwamtoga (kushoto) akimkabidhi
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) ufunguo wa
moja kati ya pikipiki 20 zilizotolewa na shirika la hilo jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akimkabidhi
Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa Kigoma Dkt. Deus
Leonard (kushoto) moja kati ya magari manne yaliyokabidhiwa kwa
Serikali kutoka kwa shirika la GLRA la Ujerumani nchini jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akisalimiana na
Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa Ilala baada ya
kumkabidhi moja kati ya magari manne yaliyokabidhiwa kwa Serikali
kutoka kwa shirika la GLRA la Ujerumani nchini jijini Dar es
salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).

Post a Comment