Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli katikati akiwa na Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada kulia wakipita
juu ya Daraja la Lugalo mara baada ya kulikagua katika ziara ya Ukaguzi wa
Barabara ya Mwenge Tegeta jijini Dar es salaam leo.
Balozi
wa Japan nchini Ndugu Masaki Okada akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said
Meck Sadick wakipanda ngazi za daraja la juu la watembea kwa miguu flyover Ubungo katika ukaguzi wa
Barabara za kupunguza Msongamano (BRT) Ubungo jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ujenzi wa kituo cha
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) Morocco jijini Dar Es Salaam
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia akiwa pamoja na
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakikagua moja ya madaraja makubwa
katika barabara ya Mwenge-Tegeta jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua daraja katika
barabara ya Mwenge - Tegeta ambayo ujenzi wake umeshakamilika.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale
aliyenyoosha mkono akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya
Mwenge-Tegeta ambao umekamilika.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza na Balozi wa
Japan Nchini Masaki Okada wakati wa Ukaguzi wa Barabara za Kupunguza msongamano
katika eneo la manzese jijini Dar es Salaam
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadick , Balozi wa Japan Masaki Okada
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakisikiliza
kwa makini maendeleo ya mradi huo.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akipita juu ya daraja la
waenda kwa miguu katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam
Post a Comment