Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja ameuwawa kikatili kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika katika eneo la mkundi manispa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo wamesema wameshuhudia kundi la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi kufuatilia tukio hilo walohusika wachukuliwe hatua.
Wananchi wakazi wa kata ya mkundi wamesema hilo sio tukio la kwanza kutokea kwa watu kuuwawa na kisha kuchomwa moto na kuomba vyomba vya sheria kufanya kazi zake kwani huenda matukio hayo yanatokana na watu kuchoshwa na baadhi ya matukio ya wizi ambayo watuhumiwa huachiwa huru na vyombo vya sheria pasipo kuchukuliwa hatua.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo .
Post a Comment