Kufuatia
kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi jirani ya Rwanda mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt,Ntuli Kapologwe amewatoa hofu wananchi wa
mkoa wa Shinyanga juu ya uvumi wa kuingia kwa ugonjwa hatari wa Ebola
mkoani Shinyanga.
Mganga
huyo wa mkoa amewatoa hofu wananchi kufuatia kuenea uvumi kuwa kuna
mgonjwa wa Ebola aliyefikishwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga
kutoka moja ya mitaa katika Manispaa ya Shinyanga.
Kwa
mujibu wa Mganga Mkuu huyo mgonjwa huyo ambaye alikuwa akitokwa damu
mdomoni na puani alifika hospitalini hapo Agosti 12 mwaka huu na mara
baada ya kufika wauguzi na madakitari walitaharuki.
Mgonjwa
alilazimika kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku baadhi ya
wauguzi na madaktari wakimkimbia hali iliyotia hofu kwa baadhi ya
wahudumu na hata wagonjwa hospitalini hapo.
Hata
hivyo Mganga Mkuu huyo alisema hakuna mgonjwa wa Ebola na kuwataka
wananchi waamini hivyo na kuwa uongozi wa mkoa umejipanga kukabiliana na
ugonjwa.
Alisema
mgonjwa aliyepokelewa ana matatizo ya kutokwa damu mara kwa mara na
kuwa baada ya uchunguzi wa awali imebainika siyo Ebola.
Hata
hivyo katika kukabaliana na ugonjwa huyo waganga wakuu katika
halmashauri zote 6 za wilaya za mkoa wamekubaliana pindi
atakapogundulika mtu mwenye dalili za ugonjwa huo taarifa itolewe mara
moja katika ngazi ya mkoa na kuna timu maalum ya kushughulika na ugonjwa
huo hatari.
Alisema
mara baada ya taarifa kutolewa timu hiyo ndiyo itakayo thibitisha kama
kweli mgojwa huyo ana dalili zote za ebola na taarifa kutolewa.
Mganga
huyo pia alisema hospitali zote katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga
zimepewa maelekezo juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Post a Comment