Yaliyomtokea Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu mwaka jana huenda yakajirudia mwaka huu baada ya kugundilika mahusiano mapya baina ya Diamond na msanii wa muziki aina ya Afro Pop na mtangazaji wa kipindi cha Dance 100% kinachorushwa kupitia kituo cha Televisheni ya vijana EATV, Menina Atick a.k.a Menina la Diva.....
Taarifa
toka vyanzo vya kuaminika zinadai kuwa Menina hivi sasa ndo
binti pekee aliyeiteka akili ya Diamond kuliko wote waliowahi
kuwa naye kimahusiano huku mama mzazi wa Diamond Bi, Snura
Kassim akionekana kumkubali kwa asilimia zote binti huyo....
Vyanzo
hivyo vimebainisha kuwa mahusiano ya Menina na Diamond
yamekuwepo kwa miezi kadhaa sasa na Diamond amekuwa na wivu
wa kupindukia juu ya demu huyo kuliko inavyosemekana kwani
amekuwa akimfuatilia kwa kila hatua....
"Hakuna
kitu anachokifanya Menina kwa sasa Diamond asijue, anampenda
vibaya utadhani karogwa na kuna kipindi Diamond alitaka kumzuia
asijihusishe na chochote kwenye Dance 100% kwa kuhofia kuporwa
lakini baadae alikubali aendelee na Dansi 100% baada ya
kuhakikishiwa na dada yake Queen Darling ambaye ni mmoja wa
majaji katika shindano hilo kwamba atamlinda asiguswe na mtu," kimesema chanzo hicho.
Habari
zaidi zinasema kwamba hata hivi majuzi( kipindi cha mwezi
mtukufu wa Ramadhani) Wema alipigwa marufuku kushiriki
maandalizi ya futari nyumbani kwa kina Diamond kwa kigezo kuwa
taratibu za dini ya kiislamu haziruhusu hawara kumpikia
mwanaume futari lakini Menina alikuwa akifanya jambo hilo kwa
kujinafasi....
"Karibu
mwezi mzima Menina alikuwa akienda kwa kina Diamond na kupika
futari, mbali ya hilo alikuwa akifanya kila alichokitaka katika
nyumba hiyo pamoja na kufanya usafi katika chumba cha
Diamond," kimesema chanzo chetu.
Hata
hivyo chanzo chetu kimesema kuwa kuna wakati Diamond aliwahi
kusikika akisema kuwa hawezi kumuoa Wema kutokana na rekodi
yake ya kuwahi kuwa na mahusiano na watu wengi wanaojulikana
nchini hivyo kuwa naye kwa ajili ya kujitangaza kimuziki(
kumpatia kiki) tu na muda wa kuoa utakapofika, ataoa binti
asiye na umaarufu jijini.....
Kibaya
zaidi ni kwamba mama Diamond ameelezwa kuwa na mapenzi ya
dhati na Menina jambo ambalo linamfanya akose raha pindi Wema
anapofika nyumbani kwake...
Diamond
alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili kuzungumzia
jambo hilo, simu yake iliita bila kupokelewa na juhudi za kumtafuta bado zinaendelea. Wema hakupatikana
katika simu zake zote.
Post a Comment