Hatimaye
mshambulzi wa Colombia James Rodriguez aliyeduwaza ulimwengu kwa
kufunga mabao mengi zaidi katika kombe la dunia lililokamilika huko
Brazil mwezi uliopita amepokea tuzo lake la mfungaji mabao mengi ''
Golden Boot''.
Rodriguez
ambaye aliyetikisa wavu mara 6 huko Brazil sasa anakibarua cha kutafuta
namba huko Real Madrid dhidi ya wakinzani wenye haiba yake kama
mchezaji bora msimu huu Christiano Ronaldo.
Rodriguez alinunuliwa na mabingwa hao wa kombe la mabingwa barani ulaya kutoka Monaco kwa pauni milioni 71.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa anamatumaini makubwa ya kutamba Santiago Bernabéu.
Bao
lake dhidi ya Uruguay katika robo fainali ya kombe la dunia limepigiwa
upatu kutwaa tuzo la bao la mashindano japo Rodriguez mwenyewe
anaikumbuka bao lake la kipekee dhidi ya Japan kuwa bora.
Colombia
ilitegemea mabao yake sita katika mechi 5 kufuzu kwa hatua ya robo
fainali kabla ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya wenyeji
Brazil.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment