Yaliyomtokea Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu mwaka jana huenda yakajirudia mwaka huu baada ya kugundilika mahusiano mapya baina ya Diamond na msanii wa muziki aina ya Afro Pop na mtangazaji wa kipindi cha Dance 100% kinachorushwa kupitia kituo cha Televisheni ya vijana EATV, Menina Atick a.k.a Menina la Diva.....
Taarifa toka vyanzo vya kuaminika zinadai kuwa Menina hivi sasa ndo binti pekee aliyeiteka akili ya Diamond kuliko wote waliowahi kuwa naye kimahusiano huku mama mzazi wa Diamond Bi, Snura Kassim akionekana kumkubali kwa asilimia zote binti huyo....
Vyanzo hivyo vimebainisha kuwa mahusiano ya Menina na Diamond yamekuwepo kwa miezi kadhaa sasa na Diamond amekuwa na wivu wa kupindukia juu ya demu huyo kuliko inavyosemekana kwani amekuwa akimfuatilia kwa kila hatua....
"Hakuna kitu anachokifanya Menina kwa sasa Diamond asijue, anampenda vibaya utadhani karogwa na kuna kipindi Diamond alitaka kumzuia asijihusishe na chochote kwenye Dance 100% kwa kuhofia kuporwa lakini baadae alikubali aendelee na Dansi 100% baada ya kuhakikishiwa na dada yake Queen Darling ambaye ni mmoja wa majaji katika shindano hilo kwamba atamlinda asiguswe na mtu," kimesema chanzo hicho.
Habari zaidi zinasema kwamba hata hivi majuzi( kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani) Wema alipigwa marufuku kushiriki maandalizi ya futari nyumbani kwa kina Diamond kwa kigezo kuwa taratibu za dini ya kiislamu haziruhusu hawara kumpikia mwanaume futari lakini Menina alikuwa akifanya jambo hilo kwa kujinafasi....
"Karibu mwezi mzima Menina alikuwa akienda kwa kina Diamond na kupika futari, mbali ya hilo alikuwa akifanya kila alichokitaka katika nyumba hiyo pamoja na kufanya usafi katika chumba cha Diamond," kimesema chanzo chetu.
Hata hivyo chanzo chetu kimesema kuwa kuna wakati Diamond aliwahi kusikika akisema kuwa hawezi kumuoa Wema kutokana na rekodi yake ya kuwahi kuwa na mahusiano na watu wengi wanaojulikana nchini hivyo kuwa naye kwa ajili ya kujitangaza kimuziki( kumpatia kiki) tu na muda wa kuoa utakapofika, ataoa binti asiye na umaarufu jijini.....
Kibaya zaidi ni kwamba mama Diamond ameelezwa kuwa na mapenzi ya dhati na Menina jambo ambalo linamfanya akose raha pindi Wema anapofika nyumbani kwake...
Diamond alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili kuzungumzia jambo hilo, simu yake iliita bila kupokelewa. Wema hakupatikana katika simu zake zote.
Post a Comment