Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JWTZ lasherehekea Miaka 50 kwa kuvisaidia vituo vya kulea watoto yatima


Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Sarah Wambali akisoma risala ya kumkamribisha Mgeni rasmi katika hafla ya kusherekea miaka 50 ya Jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam, ambapo wanatarajia kutoa misaada ya vyakula na vifaaa mbalimbali kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi ambaye ni mgeni rasmi katika hafla ya kusherekea miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania leo jijini Dar es Salaam na kuzindua wiki ya kusaidia jamii kwa kutoa msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi kushoto, akikabidhi msaada wa chumvi na baadhi vyakula kwa watoto wa kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani cha Mburahati ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi wiki ya huduma kwa Jamii inayoendeshwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania leo jijini Dar es Salaam viwanja vya Lugalo, kulia ni Mkuu wa Utumishi wa Jeshi hilo Meja Jenerali Vincent Mritaba na Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii Brigedia Jenerali Sarah Wambali.
Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Sarah Wambali akisalimiana na watoto wa kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani cha Mburahati baada ya kuwakabidhi msaada ya vyakula katikati ni mgeni rasmi Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi na kulia ni Mkuu wa Utumishi wa Jeshi hilo Meja Jenerali Vincent Mritaba leo jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na maafisa Jamii na wananchi wakifuatilia kwa makini risala ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi(hayupo katika picha), wakati wa hafla ya kufungua wiki ya kusaidia jamii ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi laWananchi wa Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi(katikati) ambaye ni mgeni ramsi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi katika hafla ya kuazimisha miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kuzindua wiki ya jamii pamoja na kutoa msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi(katikati) ambaye ni mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jamii katika hafla ya kuazimisha miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kuzindua wiki ya jamii pamoja na kutoa msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu, leo jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence Maelezo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top