Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA, WANANCHI WATAKIWA KUJIHADHALI


Pichani ni baadhi ya  Daktari wakiwa wamembeba mgonjwa wa EBORA picha kwa hisani ya Mtandao.

Na Hannah Mayige,  wa Chuo Kikuu Huria, OUT

TISHIO la ugonjwa wa Ebola unaoendelea kuuwa mamia ya watu Afrika Magharibi, umezua wasiwasi  mkubwa   kwa nchi za Afrika  na  dunia 
nzima  kwa  ujumla na  kutakiwa watanzania kuchukua tahadhari  kubwa kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.

    Lazima  Serikali na wananchi  wazingatie masharti na tahadhari inayotolewa kimataifa kuudhibiti ugonjwa na utayari wake wa kupambana nao.

    Ugonjwa wa Ebola, umekuwa tishio kubwa kwa uhai na ustawi wa mataifa mbalimbali yakiwemo ya Afrika Mashariki ambako Tanzania ni mojawapo. 
     Mpaka  sasa,  nchi  zilizoathirika  na ugonjwa  huo ni pamoja na Cameroon, Liberia na Nigeria  ambapo  tayari  zaidi  ya
watu  1,000 wamepoteza maisha.


     Eneo la Afrika mashariki,  kuna taarifa kuwa  hivi karibuni alipatikana mgonjwa  wa Ebola  katika  nchi ya  Rwanda na kwamba miaka ya nyuma milipuko iliwahi kutokea nchini Uganda.  

    Ebola  ni ugonjwa  ambao  mpaka  sasa hauna  tiba  wala   chanjo,
ambapo  huambukiza  kwa  njia  ya  hewa   au  majimaji  yatokayo
mwilini  kama  mate , jasho,  damu na kwamba mgonjwa  akigusana  na    mtu  asiye na  virusi  hivyo  basi  anaambukizwa.

    Shirika  la  Afya  Duniani  [WHO]  limetahadharisha  nchi  mbalimbali  hasa  Afrika kuchukua tahadhari  kubwa, mfano  hivi   karibuni  ndege  za shirika la  Kenya  lilishauriwa kutoendelea  na  safari  zake za  Afrika  Magharibi  kwa  kuhofia baadhi yaabiria wake  kuhamisha virusi vya Ebola na kusambaza katika eneo la Afrika Mashariki. Kenya ni mojawapo ya nchi za Afrika mashariki zenye safari nyingi za ndege kuelekea mataifambalimbali.

Kutokana na wito huo wa WHO, tayari  Korea imesitisha safari zake za ndege kwenda Kenya kwa tahadhari ya kudhibiti usambaaji wa Ebola.  Kwa kuwa ugonjwa  huo  unaambukiza kwa  njia   ya hewa     pia na majimaji  yatokayo mwilini  hata madaktari  na wauguzi   wanalazimika   kuwa na mavazi  maalum  ambayo yanafunika  mwili  mzima, kwani  hawatakiwi kugusana  kwa  namna  yeyote  ile.

     Msimamizi wa  Vituo vya Afya mipakani Tanzania, Dk. Khalid Massa, anasema vifaa hivyo ni pamoja na magauni, aproni, buti, gloves na vifaa maalum vya kuziba pua na mdomo. “Wahudumu wanatakiwa kuvaa vifaa hivyo kujikinga na maambukizi na tayari vifaa 20,000 vimepokelewa na kusambazwa katika maeneo yaliyoainishwa,” anasema Dk. Massa.

Dk. Massa, anasema kwa kushirikiana na maofisa uhamiaji wamejikita zaidi kuchunguza wasafiri wa ndege hasa wanaotokea Afrika Magharibi.  Naye, Mtaalamu wa Kudhibiti magonjwa ya mlipuko Dk. Vida Makundi,anawaasa wananchi kuripoti mapema katika vituo vya afya au kwa viongozi wa serikali za mitaaa endapo watakuwa na dalili   za ugonjwa huo.

Anazitaja dalili kubwa  ambazo  zimeelezwa  na  Shirika   la  Afya  duniani  ni pamoja  na  kuumwa   sana kichwa , kupata  homa  kali, na  hatimaye kutokwa  na damu katika  maeneo yenye  uwazi, kama vile  mdomoni, ngozi, masikioni  na sehemu za siri.

Ebola imesababisha hofu na tafrani  kubwa  kwa nchi  hasa zinazoendelea  kwa  kuua watu bila kupata tiba ikiwa ni pamoja na madaktari  na udhoofisha  hali  ya  uchumi  kutokana na shughuli nyingi za kusafiri na
zinazokutanisha watu kusitishwa.

Shughuli za biashara za kimataifa pia  zinaendelea kutetereka kuogopa maambukizi  ya virusi  vya Ebola hasa  wananchi katika  nchi zenye  ugonjwa  huo kuogopana wenyewe  kwa wenyewe.

Mfano, huko Cameroun,  kuna  mtu alikutwa amekufa  barabarani hakuna  mtu   aliyethubutu kumsogelea  mpaka walipokuja  madaktari ambao walivalia  rasmi kuhakikisha   hakuna maambukizimapya kwa watu wengine.

Hapa  Tanzania, tayari serikali kupitia   viongozi mbalimbali akiwemo  Makamu wa  Rais Mohamed  Ali  Bilal , Waziri wa Afya Dk. Seif Rashid na baadhi ya wakuu wa mikoa ya Manyara, Dar es Salaam na  Mbeya  wamewataka wananchi kuwa  waangalifu na wageni wasio wajua   na  kuwa tahadharisha  kwenda  hospitali mara  wanapoona wana dalili  zisizo
za  kawaida  au zinazoashiria  ugonjwa
wa Ebola.

Kulingana  na tamko la serikali ,  Ebola  bado haijaingia nchini lakini  usemi wa  Kiswahili usemao ‘ ukiona mwenzako  ananyolewa,  wewe  tia maji’.
Kwa  upande wa kutenga maeneo maalum ya kushughulikia wagonjwa wa Ebola, serikali imetenga maeneo mawili kwa Dare s Salaam, Temeke na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 Waziri wa afya  DK.  Seif Rashid anasema tayari wauguzi na madaktari wanapatiwa elimu  kuhusiana  na kuudhibiti  ugonjwa wa  Ebola  kabla  haujaingia  nchini, elimu hiyo  inatolewa  katika  hospitali zote .

Nao, wananchi kwa nyakati tofauti wameendelea kumlilia mungu kwa mlipuko wa magonjwa hapa barani Afrika. “Mara ukimwi, mara Dengue mara Ebola yote hakuna tiba,” analalamika mmoja wa wananchi Kasian Komba mkazi wa Songea. 

Kutokana na taarifa za baadhi ya wananchi wa Liberia kuvamia kituo kilichotengwa kuhudumia wagonjwa wa Ebola na kupora magodoro, vifaa na wagonjwa kutawanyika, ni taarifa mbaya na huenda imetokana na kukosa elimu ya ugonjwa huo.

       Kwakuwa elimu ni muhimu,  ni vyema serikali hapa nchini ikatumia fursa hii kuelimisha umma kwa kutumia mikutano ya hadhara, Sanaa za
maonesho, mabango, vyombo vya habari kama mitandao ya kijamii,  redio, televisheni, magazeti na vipeperushi ili jamii ipate uelewa.

Makala hii imeandikwa na Hannah Mayige, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania – OUT. Anapatikana kwa E-mail  hannahmayige@gmail.com
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top