KUMEKUCHA! Miss
Kinondoni anayemaliza muda wake, Lucy Tomeka, ametamba ni lazima mrembo wa
Redd’s Miss Tanzania mwaka huu atoke Kinondoni.
Lucy alisema
ana uhakika huo mkubwa kutokana na kuwaona washiriki wa Redd’s Miss Kinondoni
na kuona wana vigezo vyote vya kulitwaa taji hilo. Mrembo huyo
ambaye atakabidhi taji la Redd’s Miss Kinondoni mwishoni mwa wiki alisema, ana
uhakika huo kutokana na uzoefu alioupata wakati akishiriki Redd’s Miss Kinondoni.
“Taji lazima
lirudi nyumbani, warembo wa Kinondoni kusema kweli wana sifa zote, wana kila
aina ya sifa. Tena mwaka huu naona upinzani ni mkali zaidi kuliko miaka yote,
kutokana na sifa ya warembo hao,” alisema Lucy.
Naye Mratibu wa
Redd’s Miss Kinondoni, Husna Maulid, alisema warembo 20 wanatarajiwa kuchuana
Ijumaa wiki hii ili kumpata mshindi kati yao. “Ijumaa fitina
yote inaisha, kinachosubiriwa ni siku tu na warembo 20 wapo katika mazoezi
makali kwa ajili ya shindano hilo.”
Shindano la
Redd’s Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Escape 1 uliopo
Mikocheni, Dar es Salaam huku kukiwa na burudani kali toka Malaika Band
inayoongozwa na Christian Bella. Taji la Redd’s
Miss Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na
aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.
Warembo
wanaoshiriki shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian
Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh
30,000 viti maalumu.
Wadhamini wa
shindano hilo ni Redd’s Original, Kitwe General Traders, CXC Africa, Jambo Leo,
Clouds FM, Michuzi Media Group, Father Kidevu, Greaters Salon, EFM na Mseto.
Post a Comment