Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati akifungua Kongamano la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la tatu la Kimataifa la Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES). Aidha Kongamano hilo lililoshirikisha jumla ya wajumbe zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi pia, litajadili usimamizi wa Rasilimali mbalimbali zikiwemo Mafuta na Gesi.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akizungumza katika
Kongamano hilo kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Picha na OMR
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, akizungumza katika
Kongamano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufungua kongamano hilo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati akifungua Kongamano la siku tatu
la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali
yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania
imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la tatu la Kimataifa la
Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES). Aidha Kongamano hilo
lililoshirikisha jumla ya wajumbe zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya
nchi pia, litajadili usimamizi wa Rasilimali mbalimbali zikiwemo Mafuta
na Gesi. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya sanamu la mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa
Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi
Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana,
linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini,
linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo. Picha na OMR
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akipokea zawadi ya
picha ya mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana
Duniani (YES), Meng Wang, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo, la
siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala
mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal (kushoto) ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi ya ramani ya Afrika, Rais wa wa Mtandao wa
Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi
Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana,
linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini,
linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo,
baada ya ufunguzi. Picha na OMR
Baadhi
ya wanafunzi kutoka katika sekondari mbalimbali jijini Dar es Salaam
katika picha ya pamoja na Makam wa Rais Makam wa Rais Makam wa Rais Dk.
Mohamed Gharib Bilal, pamoja na viongozi wengine, akiwemo Rais Mstaafu
wa Awamu wa pili Benjamin Mkapa, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo na viongozi wengine waliohuduria mkutano huo.
Makam
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimpa zawadi ya kinyago Mwenyekiti wa
vijana wanasayansi kwa upande wa Tanzania Steven Nyagonda,
anayefuatilia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Vijana wanasayansi duniani wametakiwa kutoka na njia mbadala kupitia tafiti wanazofanya katika tasnia ya jiolojia ili zisaidie katika kuendeleza rasilimali duniani hususan barani Afrika na hatimaye ziweze kulinufaisha bara hilo na kuleta maendeleo endelevu.
Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akifungua mkutano wa tatu wa vijana wanasayansi duniani unaoendelea jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, vijana wanasayansi wanayo nafasi kubwa ya kuleta mabadililiko kupitia rasilimali mbalimbali zilizopo Afrika yakiwemo madini, mafuta , gesi asilia na rasilimali nyingine.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa azitaka nchi za Afrika kuwapa nafasi vijana
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya pili, Benjamin Mkapa amezitaka serikali za nchi za Afrika kuipa kipaumbele cha pekee elimu kwa vijana wanasayansi pamoja na kuwapa nafasi kuonesha na kutoa ufumbuzi kutokana na tafiti mbalimbali wanazozifanya ili kuweza kuziendeleza rasilimali zilizopo barani Afrika.
Profesa Muhongo aeleza Afrika ni bara la kizazi kijacho
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, Afrika ni bara la kizazi kijacho, na kuongeza kuwa, vijana wanasayansi wanayo nafasi kubwa kuleta mabadiliko na kuendeleza rasilimali zilizopo Afrika kwa ajili ya kizazi kijacho.
Vilevile Profesa Mihongo amezitaka Serikali barani Afrika kuwekeza kwa vijana ili kuweza kupata wataalam waliobobea huku akitolea mfano Tanzania kuwa, dhamira ya Serikali kufikia mwaka 2025 ni kuhakikisha kwamba Tanzania inahesabika kuwa miongoni mwa nchi zenye kipato cha kati kupitia rasilimali za mafuta na gesi asilia. Hivyo uwepo wa wataalamu waliobobea katika taaluma hiyo ni muhimu.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma, ameeleza kuwa, ni fursa nzuri kwa vijana kujifunza kutoka kwa wajiolojia waliobobea, jambo ambalo litawasaidi kufuata nyendo za wataalam hao. Ameongeza kuwa, kupitia uzoefu ambao vijana hao wataupata, utasaidia katika kufanikisha masuala mbalimbali ya kiuchumi na kuinua nchi zao kutokana na taaluma hiyo.
Vilevile, ametoa pongezi kubwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kuirithisha taaluma hiyo kwa vijana wa Tanzania, Afrika na duniani kupitia nafasi mbalimbali ambazo amekuwa kiongozi kupitia taaluma hiyo ikiwa ni pamoja na kuongoza Wizara ya nishati na Madini.
Kwa upande wake Rais wa vijana wanasayansi duniani, Meng Wang, ameeleza kuwa hii ni nafasi kwao ya kuwasilisha tafiti uzoefu, changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Aidha, ameongeza ni fursa kwa Afrika ikizingatiwa kuwa, mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza barani humo.

Post a Comment